Besigye kitanzini na mahakama za kijeshi Uganda

Mpinzani wa Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa na mahakama ya kijeshi nchini humo kwa makosa manne likiwemo la kupatikana na silaha.

Kanali Mstaafu Dkt. Kizza Besigye Kifeefe alizaliwa mwaka 1956 katika wilaya ya Rukungiri, magharibi mwa Uganda.

Besigye alifuzu kama daktari baada ya kusomea Chuo Kikuu cha Makerere, mjini Kampala.

Alijiunga na Chama cha Museveni cha Uganda Patriotic Movement muda mfupi baada ya kuondolewa madarakani kwa Idi Amin 1978.

Mwaka 1982, alijiunga na Museveni vitani baada ya kuzuiliwa miezi miwili katika hoteli moja mjini Kampala akituhumiwa kushirikiana na waasi.

Baada ya Museveni kuingia uongozini, alimteua Dkt. Besigye, wakati huo akiwa na umri wa miaka 29, kuwa waziri wa nchi aliyesimamia masuala ya ndani na masuala ya siasa za taifa.

Dkt Besigye alipanda cheo jeshini na kufikia cheo cha kanali.

Alistaafu muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2001, miezi michache kabla ya kujitokeza na kutangaza kwamba angewania urais.

Besigye husifiwa sana kutokana na moyo anaoonyesha anapotoa hotuba zake na wengi wamemsifu kwa kusimama na kupinga utawala wa Museveni.

Post a Comment

0 Comments