DEO MUSHI:BILIONI 3.6 KUKARABATI MFEREJI WA MAKARESHO,

 


KIBOSHO MAGHARIBI-MOSHI

MGOMBEA  wa Kiti cha Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Kata ya Kibosho Magharibi katika Jimbo la Moshi Vijijini,.Deogratias  Francis Mushi,amesema serikali ya Chama cha mapinduzi,imeutengea shilingi Bilioni 3.6 mfereji wa Makeresho kwa ajili ya kuufanyia ukarabati mkubwa ili kuwezesha wananchi wa kata hiyo kunufaika na kilimo cha umwagiliaji.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Manushi Ndoo katika moja ya mikutano yake ya kampeni  kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na madiwani jumatano Ijayo,Deo amesema mfereji huo ni kichocheo kikubwa katika shughuli za kilimo kwa wananchi hao.

Amesema mfereji huo ni moja ya vipaumbele vilivyomo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025/2030 ikiwamo pia ukarabati wa barabara za ndani ikiwa ni mkakati wa serikali ya CCM kuhakikisha wananchi wanaendesha shughuli zao ikiwamo usafrishaji wa mazao bila usumbufu.

Amesema mara baaada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa kata hiyo atahakikisha visima virefu vitatu vinachimbwa katika maeneo ya Kombo,Ufuni na Onana ili kuwawezesha wananchi kuendesha kilimo cha umwagiliaji. 

Deo Mushi ambaye amepita bila kupingwa kwenye kata hiyo akisuburia wananchi wampigie kura nyingi za ndiyo,anarudi tena kwenye kata hiyo baada ya kuwa Diwani mwaka 2015 hadi 2020.

Katika kipindi hicho cha Miaka mitano alitekeleza ipasavyo Ilani ya uchaguzi ya CCM katika sekta ya kilimo,elimu,uboreshaji wa miundimbinu ya barabara,maji afya,ustawi wa jamii,kuimarisha vikundi vya kinamama,vijana na watu wenye ulemavu,kusaidia wazee,wajane pamoja na kuimarisha michezo.

Aliwaomba wananchi wa kata hiyo pamoja na wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi siku ya upigaji kura na kukipa kura nyingi chama cha mapinduzi kwa ngazi ya Rais,wabunge na madiwani na kuongeza kuwa mtaji wa CCM ni wanaCCM wenyewe.

Kuhusu kuwawezesha wananchi wa kata yake kiuchumi,alisema kama wananchi watampigia kura nyingi za ndiyo atakwenda kwenye Baraza la madiwani na kuhakikisha mikopo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu inawafikia kwa wakati. 

Mkutano huo wa kampeni ulitanguliwa na elimu juu ya uanzishaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo ufugaji wa Ng;ombe wa maziwa,kuku pamoja na kilimo ambako baadhi ya vikundi vilivyoandikishwa vilishiriki darasa hilo,

Mgombea huyo wa kiti cha udiwani pia ameahidi kurejesha michezo kwa vijana wa kata hivyo ambako watashiriki micvhezo mbali mbali kwa kushindanishwa na kata za jirani ikiwamo Kibosho Mashariki lengo ni kuibua vipaji na kupunguza vitendo vya kiharifu








Post a Comment

0 Comments