Profesa Ndakidemi aipa Milioni 5
familia iliyopoteza watu wanne kwenye mafuriko Kata ya Kimochi
Mvua hiyo ambayo ilileta
uharibifu mkubwa Katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Kilimanjaro ilisababisha
mafuriko ambayo yaliharibu Mali za watu zikiwamo nyumba ,mifugo,vyakula.
Profesa Ndakidemi alitoa ahadi
hiyo wakati wa mazishi ya watu hao Katika kata ya Kimochi jimboni humo.
Alisema kiasi hicho cha fedha
kitatumika kuwarejeshea makazi yao baada ya nyumba Yao kuanguka na kukosa
makazi.
Katika mazishi hayo,Profesa
Ndakidemi alitoa ubani wa shilingi laki tano kwa familia hiyo huku akitoa tani
mbili za mahidi kwa wananchi wa Kata za Mabogini na Arusha chini ambazo
ziliathiriwa na mafuriko hayo.
Mwenyekiti wa ukoo wa
Mchaki,Elikunda Chaki amesema profesa Ndakidemi alitimiza ahadi yake Agosti 21
mwaka huu kupitia kwa Katibu wake,Alois Robert.
"Ni kweli mheshimiwa mbunge
alimiza ahadi yake na sisi kama familia tumemshukuru kwa kukamilisha ahadi
yake",amesema Chaki.
Septemba 11 mwaka huu familia
hiyo ya Chaki ikamwandilia barua ya shukrani Profesa Ndakidemi kutokana na
kutimiza ahadi yake.
"Mhe.Mbunge wa Moshi
Vijijini husika na mada tajwa hapo juu,sisi wanafamilia wa familia hizi mbili
tunapenda kuleta shukrani za kipekee kwa kwa mchango wako uliowezesha ujenzi wa
nyumba kwa ndugu zetu katika maafa ya mafuriko katika kata ya Kimochi ,kijiji cha
Lyakombilo".
Familia hiyo ikahitimisha salama
za pongezi kwa mbunge huyo kwa kunukuu maandiko matakatifu kutoka kitabu cha
Mathayo sura ya 25 mstari wa 40 na hapa nanukuu
"Na mfalme
akajibu,akawaambia Amin nawaambia kadri mlivyomtendea mmojawapo na hao ndugu
zangu waliowadogo,mlinitendea mimi ".mwisho wa kunukuu.
Zaidi ya watu 4,000 wariripotiwa
kuathiriwa na mafuriko hayo yaliyosabishwa na mvua kubwa zilizokuwa zikiendelea
kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro.
Mbali na hao zaidi ya Kaya 906
ziriripotiwa kuathiriwa na mafuriko hayo huku watu sita wakiripotiwa kufariki
dunia kutokana na mvua hizo.

0 Comments