HILI NI JENGO LA UKUMBI WA MIKUTANO KIRIMA BORO AMCOS,UJENZI WAKE UNAHOJIWA NA WANACHAMA KWAMBA NANI ANAJENGA NA KWA GHARAMA YA SH,NGAPI NA MKATABA WA UJENZI UNASEMAJE
KUMEKUCHA,naam ndivyo unavyoweza kusema baada ya kelele nyingi za wanaushirika wa Chama Cha msingi cha Ushirika wa mazao cha Kirima Boro Amcos kupaza sauti juu ya uuzwaji holela wa ardhi ya ushirika,kelele hizo sasa zimepata ufumbuzi.
Ni hivi ,Tume ya maendeleo ya ushirika nchini kupitia Mrajis wa ushirika nchini ,Dkt,Benson Ndiege imetuma timu ya uchuguzi kwenye chama hicho kuchunguza malalamiko ya wanaushirika hao juu ya mwenendo usioridhisha wa Bodi ya uangalizi ambayo imeweka pembeni makujumu iliyopewa na kujikita kuuza ardhi ya ushirika kama mali za ukoo maarufu kama vihamba.
Novemba 11 mwaka huu kadama24blog tuliandika kwa kirefu malalamiko ya wanaushirika hao kwamba ardhi yao inauzwa kwa watu mbali mbali wakiwamo wanasiasa,wafanyabiashara na watumishi wa umma.
Taarifa kutoka Kirima Boro Amcos zinaeleza kuwa Alhamis ya Desemba 11 mwaka huu ilikuwa ufanyike uchaguzi wa kuchagua Bodi mpya lakini Mrajis msaidizi alipoingia ukumbini alitangaza kufuta uchaguzi huo ili kupisha uchunguzi unaoendelea hatua iliyozua sintofahamu na mwisho bodi ya zamani ikarejeshwa kuendlea kufanyakazi japo kwa masharti magumu wakti mchakato wa uchaguzi wa Bodi ya kudumu ukifanyika .
Kabla ya wajumbe kuingia ukumbini walionekana kwenye maeneo mbalimbali ya kuuza vileo wakiburudika na kinywaji ,vinywaji ambavyo inadaiwa vilikuwa vikilipiwa na viongozi wa bodi ya uangalizi wakiamini watachaguliwa kuendelea na uongozi.
Hata hivyo kabla ya uchaguzi huo Mrajis msaidizi aliulizwa juu ya malalamiko ya wanaushirika kufumbia macho ufisadi unaofanywa na viongozi hao wa kuuza ardhi ya ushirika.
"Madai mengine ni kwamba mmeshindwa kusimamia kufanyika kwa ukaguzi wa mahesabu ya chama na mmeshindwa kusimamia uchaguzi wa vingozi wa kudumu,nini kauli yako?
Mrajis msaidizi alijibu ujumbe wetu na haya ndiyo majibu yake
"Hoja zilishawasilishwa Takukuru kwa hatua,tarehe ya uchaguzi ilishapangwa na walishatangaziwa ni tarehe 11/12/2025"
"Ukaguzi..chama kimekaguliwa kuishia msimu wa 2024/2025,msimu wa 2025/2026 ndo huu wanaoishi nao"
"Ni vyema ukafika chamani ukapata zaidi kuhusu hoja zilizotolewa ili u ballance story "
1.matangazo ya uchaguzi
2.taarifa ya ukaguzi husika
3.mauzo ya trekta
4.uuzwaji wa maeneo
Majibu yote yapo wazi
hayo ndiyo majibu ya mrajis msaidizi kulingana na maswali yetu na kusitishwa kwa uchaguzi huo na kuanza kwa uchunguzi huo ni dhahiri Tume ya maendeleo ya ushirika nchini imeona msingi wa malalamiko ya wanaushirika.
Kwa wale ambao hawakubahatika kusoma habari yetu ya awali ya Novemba 11 basi tunairejea hapa kwa faida ya wadau wetu.
WANACHAMA wa Chama cha msingi cha ushirika wa mazao cha Kirima Boro Amcos kilichopo wilaya ya moshi Vijijini,wamepaza sauti kwa mamlaka za uchunguzi kupiga kambi kwenye ofisi za chama hicho na kufanya uchuguzi juu ya madai ya viongozi wa muda wa chama hicho kudaiwa kuuza mashamba ya chama hicho kama ardhi ya ukoo maarufu kama vihamba kwa lugha ya kabila la Kichagga.
Wanadai kuwa viongozi hao wamewauzia ardhi ya chama hicho watu mbalimbali wakiwamo wanasiasa,wafanyabiashara wakubwa na watumishi wa umma jambo ambalo wanadai haliendani na sera ya serikali katika mkakati wa kuendeleza ushirika nchini.
Timu yetu ya uchunguzi iliyopiga kambi kwenye ushirika huo imeibua mengi ambayo bado tunayafanyia uchunguzi ikiwamo majina ya waliouziwa ardhi hiyo Pamoja na kuwatafuta mmoja baada ya mwingine ili kupata kauli zao juu ya kuuziwa ardhi ya wanaushrika.
Kwa faida ya wasomaji wetru,machi 21 mwaka 1967 vyama viwili vya msingi vya ushirika vya Kimasio na Kirima Boro viliandika barua ya kuomba kununua shamba lililokuwa likimiliwa na raia mmoja wa kigeni Tsoucas baada ya kubaini kuwa shamba hilo haliendelezwi .
“Vyama viwili vilivyotajwa hapo juu vinayo heshima kubwa kununua shamba hilo kwa manufaa ya watu wote,baada ya uchunguzi mwingi kwa wahusikao na shamba hilo ilionekana kuwa liko chini ya ulinzi wa manager wa Standard Bank”,inasema barua hiyo na kuongeza.
“Baada ya kumwona manager wa Bank alitoa dokezo kuwa shamba hilo ni ekari 450 na ni jumla ya sh,600,000,kwa kifupi,shamba hilo halina mastawisho yeyote bali kuna vyumba viwili tu(2),zaidi ya hapo tulikwisha julishwa kuwa alikuwa na deni la Bank jumla ya sh,15,000”.
Kuambatana na kima hicho cha sh,600,000,tunakuomba shamba hilo lichukuliwe kama bei hiyo ni ya halali,tunatumai kuwa ombi letu hili litafikiriwa kwa makini”,imehitimisha barua hiyo ambayo nakala yake timu yetu ya uchunguzi inayo .
JENGO LA OFISI ZA CHAMA CHA MSINGI CHA USHIRIKA CHA KIRIMA BORO AMCOS KAMA LINAVYOONEKANA
Kulingana na uchunguzi wetu,Desemba 14 mwaka 2023 mwenyekiti wa Kijiji cha Boro,Laurent Mushi kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho alimwandikia barua mkuu wa wilaya ya Moshi akilalamikia mwenendo wa uongozi huo kuuza ardhi ya shamba la ushirika kama vihamba akimuomba kuingilia kati lalamiko hilo na kumuomba azuie mpango wa kugawa ardhi ya ushirika.
“Mh.Mkuu wa wilaya baadhi ya wanakijiji wenye nia njema ya kudumisha amani wanakuomba uingilie kati lalamiko hili na kuzuia mpango wa kugawa ardhi ya Ushirika inayosimamiwa na Chama cha ushirika cha msingi cha Kirima Boro”.
Uratibu wa kumilikisha vipande vidogo vidogo vya ardhi usimame na badala yake eneo libaki kwa ajili ya Taasisi muhimu kwa umma mfano;Kituo cha Afya,Kituo cha Polsi Chuo cha ufundi n.k”.
“Wanakijiji wamenieleza kuwa hofu yao ni kwamba mpango huu ukifanyika bila kuweka utaratibu wa kisheria wa kumilikisha ardhi ambayo ni mali ya Ushirika,viashiria vya ugomvi vinaweza kutokea katika shamba na kusababisha uvunjifu wa amani siyo tu kwa wanachama wa chama cha Ushirika cha msingi bali pia kwa wakulima ambao baba zao au mama zao ndio waliochangia fedha za kununua ardhi hiyo mwaka 1967 kutoka kwa wamiliki wa kigeni na wamekuwa wakijiuliza maswali yafuatayo…….”
Pamoja na kelele hizo kasi ya kuuzwa wa ardhi ya ushirika inazidi kushika kasi,
Je ni kina nani wanuza ardhi hiyo?
Je ni kina nani wameuziwa ardhi hiyo,usikose makala zetu hapo baadae
.jpg)
.jpg)
0 Comments