DEO MUSHI 'MWAMBA WA KIBOSHO'APIGIWA CHAPUO UENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI

 


                                                               KIBOSHO MAGHARIBI -MOSHI 

WANANCHI wa kata ya Kibosho Magharibi wametuma salamu kwa madiwani na wabunge wawili wanaounda halmashauri ya wilaya ya Moshi(Moshi DC)wakipendekeza Diwani mteule anayesubiria kuapishwa kuwa Diwani wa kata hiyo Deo Mushi apeperushe bendera ya mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Halmashauri ya wilaya ya Moshi inaundwa na majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Vunjo na Moshi Vijijini na katika Baraza la madiwani lililopita mwenyekiti wa halmashauri hiyo alikuwa Morris Makoi akitokea kata ya Okaoni na sasa anagombea kiti cha Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha mapinduzi(CCM)jimbo la Moshi Vijijini.

Upatu huo wa kumtaka Deo Mushi awe mwenyekiti wa halmashauri hiyo ulianza kupigwa kitambo na juzi juzi wakati wa mkutano wa Kampeni za udiwani katika Kijiji cha Manushi Ndoo,mwananchi mmoja alinyoosha mkono akiomba kuzungumza na alipopewa kipaza sauti alianza kumwagia sifa kada huyo wa CCM akidai anauzoefu wa kutosha kuweza kushika nafasi hiyo.

“Nakuomba sana mheshimiwa Morris Makoi ile nafasi yako ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya umwachie kaka yetu Deo Mushi,tunamwamini anauzoefu mkubwa wa kuongoza halmashauri hiyo,tunakuomba sana”,alisema mama huyo Agustina Faustine Munishi huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi waliojiotokeza katika mkutano huo.

Joto la kuwania nafasi hiyo ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi linazidi kupanda kila uchao hata kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani utakaofanyika jumatano ya Oktoba 29 ambako madiwani wanaotoka upande wa jimbo la Vunjo nako moto ukiwaka wa nani apeperushe bendera hiyo kutokea upande huo.

Kwenye mkutano huo wananchi walipewa nafasi ya kuzungumzia kero zao katika kata hiyo na baadhi yao wakatoa kilio chao juu ya uhaba wa walimu katika baadhi ya shule zao za msingi hatua ambayo imewafanya kutoa fedha mara kwa mara kwa ajili ya kulipia malipo ya walimu wa kujitolea..

Kilio kingine cha wananchi wa kata hiyo ni kupewa Ankara kubwa za maji ambazo haziendani na uhalisia wa matumizi ya maji hoja iliyoungwa mkono na mgombea huyo wa kiti cha udiwani na kuahidi kushughulikia kero hiyo mara tu atakachaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo.

Akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa kampeni,Deo Mushi alisema Ankara za maji zimekuwa kero kubwa kwa wananhi wa kata hiyo na ameahidi kushuhulikia kero hiyo ambayo imekuwa ni ya muda mrefu kwa wananchi hao.

Aliwataka wananchi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuwaomba kumpigia kura nyingi mgombea wa kiti cha urais kupitia Chama cha mapidunzi(CCM),Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,mgombea kiti cha ubunge jimbo hilo,Morris Makio nay eye mwenyewe ili kujenga utatu mtakatifu au mafiga matatu,




Post a Comment

0 Comments