Ofisa
mfawidhi wa LATRA mkoa wa Kilimanjaro,Paul Nyello ameeleza hayo kwa waandishi
wa habari akiwa katika kituo kikuu cha mabasi mjini moshi akiwa katika zoezi la
ukaguzi na kuangalia hali ya usafiri.
“Nipende kuchukua
nafasi hii kutoa tathimini fupi ya hali ya usafiri ndani ya mkoa wetu wa Kilimanjaro
kwa maana ya wilaya za Same,Mwanga,Rombo Hai na Siha hali ya usafri ni nzuri na kwa
upande wa bajaj na Taksi huduma zinaendelea vizuri”,alisema.
Alisema pia
usafiri wa nje ya mkoa kwa maana ya mabasi yaendayo mji wa Arusha usafiri pia
umeimarika na hata mabasi ya masafa marefu kutoka Moshi kwenda mkoa wa
Geita kupitia Singida,Tabora na Shinyanga huduma zimeanza kurejea na kuahidi
hali kuendelea kuwa tulivu zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda.
Alitaja njia nyingine za mabasi kuwa ni kutoka Moshi kwenda Tunduma mkoani Songwe pamoja na kutoka Moshi kwenda Dar es salaam usafiri umerejea huku safari za usiku nazo zikianza na hii yote ni kutokana na kuendelea kuimarika kwa hali ya usalama pamoja na kuwepo kwa hali ya utulivu.
Ofisa Mfawidhi Mamlaka ya Udhibiti usafiri Ardhini(LATRA)mkoa wa Kilimanjaro,Paul Nyello(kulia)akizungumza na waandishi wa habari katika kituo kikuu cha mabasi mjini moshi.Jumatatu ya
Novemba 3 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan na
makamu wake wa Rais,Dkt.Emmanuel John Nchimbi waliapishwa mjini Dodoma baada ya
Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi kumtangaza mshindi wa kiti cha urais baada ya
kupata kura 31.913,866 sawa na aslimia 97.76.
Katika
hotuba yake kwa taifa,Rais samia alihitimisha hotuba yake kuagiza wananchi
kuendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida na kuelekeza kamati za ulinzi
na usalama za wilaya na mikoa nchini kuendelea kuimarisha hali ya usalama.
Huduma
nyingi katika baadhi ya mikoa nchini zilisimama kutokana na kuibuka kwa ghasia
za maandamano siku ya uchaguzi mkuu oktoba 29 mwaka huu hali iliyotatiza
shughuuli za kiuchumi na baada ya maagizo ya rais huduma nyingi kwa sasa
zimerejea katika hali yake ya kawaida.
Baadhi ya wasafrishaji wa abiria katika kituo hicho cha mabasi mjini moshi wameipongeza serikali kwa kurejesha huduma zilizokuwa zimesimama kwa muda na kuitaka kuendelea kuimarisha hali ya usalama ili waendelee na shughuli za uzalishaji mali kwa amani.
Mmoja wa mawakala wa mabasi yaendayo mikoani katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi akizungumza na waandishi wa habari siku moja baada ya huduma za usafrishaji kurejea katika hali yake ya kawaidaPaul Nyello,Ofisa Mfawidhi Mamlaka ya Udhibiti usafiri Ardhini (LATRA)mkoa wa Kilimanjaro akiwa katika kituo kikuu cha mabasi mjini moshi kukagua hali ya usafiri






0 Comments