Nurdin Babu,mkuu wa mkoa wa Kilimanajro
KILIMANJARO-TANZANIA
SERIKALI imewahikikishia wananchi wa mkoa wa
Kilimanjaro kuwa uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu utafanyika ktika hali ya amani na utulivu wa hali
ya juu kwa aslimia mia moja na kuwaonya wote wanaojiandaa kuvuruga uchaguzi huo
kuwa watakabiliwa na mkono wa dola.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Oktoba 19,2025 ofisini kwake,Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro,Nurdin Hassan Babu amesema hadi sasa hali ya usalama katika mkoa wake ni shwari na
wananchi wapo tayari kwa uchaguzi mkuu.
Alitoa wito
kwa wananchi wote waliojiandikisha kupiga kura kutumia haki yao ya kikatiba kujitokeza kwenda kupiga kura bila hofu na
bila woga wowote na kwamba mara baada ya kupiga kura waendelee na shughuli zao
kwani matokeo ya kura yatabandikwa kwenye mbao za matangazo.
“Tumewaita
tuwape taarifa kwamba,wananchi ifikapo terehe 29 mwezi wa kumi siku kumi
kuanzia leo wananchi wote waliojiandikisha kupiga kura waende kwenye vituo bila
wasiwasi na bila hofu yoyote”,alisema.
“Sasa yapo mambo
mengi ya mitandaoni ,wananchi hayo naomba wayaache,mimi kama mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama nawahakikisha usalama kwa aslimia mia moja,baada ya kupiga kura
kila mwanachi aende kwenye shughuli zake za kujiletea maendeleo”
“Kama kuna
mtu amejipanga vizuri na ana misuri mikubwa tutamuona huko mbele,ninachoweza
kuwahakikisha wananchi wa mkoa wa kilimanajro uchaguzi huu kwa mkoa wa
kilimanjaro utafanyika katika hali ya utulivu na haijawahi kutokea”,amesema.
Kumekuwepo
na taarifa za watu kupitia mitandao ya kijamii kutishia kuandamana kwa lengo la
kuvuruga mchakato mzima wa zoezi la upigaji kura kwa maslahi yao binafsi
kitendo ambacho serikali na vyombo vya ulinzi na usalama vimeendelea kuonya kuwa haitowavumilia watu wa aina
hiyo.
Mamlaka ya
mawasiliano Tanzania(TCRA)kwa upande wake imekuwa ikitoa wito kwa watanzania na
watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo vizuri na kuacha kuitumia
kwa misingi isiyokuwa sahihi.
Vyama mbali
mbali vya siasa nchini vipo katika kampeni za kunadi sera kwa wananchi kuomba
ridhaa ya kuchaguliwa hapo oktoba 29 kampeni ambazo zilianza septemba 28 mwaka
huu na zitahitimishwa Oktoba 28 mwaka huu na siku inayofuata Taifa litakuwa
linaingia kwenye uchaguzi mkuu.
Viongozi mbali mbali wa dini na makundi mengine ya kijamii wameendelea kuwataka watanzania kuendelea kuenzi na kudumisha amani iliyoachwa na waasisi wa taifa hili akiwamo Baba wa Taifa Hayati Mwlimu Julius Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Babu akiwa na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wakati wamkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake leo Oktoba 19,2025


.jpg)
0 Comments