DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Kimataifa ya Kimarekani ya Neolife International imeandaa mkutano wa siku moja wenye lengo la kutoa mafunzo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara yakilenga kuwasaidia kuinua uchumi,kuendesha kilimo chenye tija pamoja na suala zima la afya.
Mkutano huo mkubwa unatarajia kufanyika kwa siku moja mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwenye Hotel ya kitalii ya Kilimanjaro Crane’s na kushirikisha wafanyabiashara kutoka maeneo mbali mbali ya mkoa huo.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo hapa Tanzania Diswa Zongo anasema lengo la kampuni hiyo ni kuifanya dunia kuwa sehemu yenye Furaha na Afya bora
“ Kampuni yetu imeanzishwa tangu 1958 huko Marekani na hapa Tanzania ipo tangu 1999 hivyo tuna zaidi ya miaka 25 hapa nchini na mkutano huu ni wa biashara wenye dhumuni la kusaidia kuinua uchumi, Afya bora na kilimo chenye tija”,amesema.
Akatoa wito kwa wafanyabiashara na wajasiriamali na jamii ya wanamoshi kushiriki mkutano huo ili kujifunza namna ya kuimarisha uchumi , Afya na zaidi kwa wakulima kulima kilimo chenye tija yaani kilimo chenye faida.
DISWA ZONGO MKURUGENZI WA NEOLIFE INTERNATIONAL TANZANIA


0 Comments