KCMC YAUNGANA NA WHO MAADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI DUNIANI

 

 Zoezi la upimaji wa afya likiendelea katika viwanja vya Hospital ya Rufaa ya Kanda ya KCMC ikiwa ni sehemu ya maadhimiho ya siku ya kisukarti duniani  

 


NOVEMBA 14 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya kisukari ikilenga kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa wa kisukari na namna ya kuuzuia na kuudhibiti katika kuboresha ustawi wa afya. 

Hospital ya Rufaa ya KCMC nayo iliungana na  Shirika la Afya Duniani (WHO) kuadhimisha siku ya Kisukari Duniani ambako iliendesha zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi katika viwanja vya Hospital hiyo kubwa katika ukanda wa kaskazini. 

 Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospital hiyo,Nyasatu Chamba anasema kaulimbiu ya mwaka huu ni “kisukari na Ustawi wa Afya chukua hatua kudhibiti kisukari pahala pa kazi” 

Anasema kaulimbiu hiyo inasisitiza umuhimu wa Taasisi, waajiri na wafanyakazi kushirikiana kutengeneza mazingira rafiki ya kazi yanayohamasisha ulaji bora, mazoezi, kupunguza msongo wa mawazo na kufuatilia afya mara kwa mara. 

“Wataalamu wetu wanaendelea kutoa elimu katika jamii hususani kwenye vyombo vya habari, katika masoko na shuleni ili kuhakikisha kila mmoja anapata uelewa sahihi kuhusu kisukari ugonjwa usio na dalili za awali kwa baadhi ya watu, lakini una madhara makubwa endapo hautadhibitiwa mapema”,anasema. 

Anataja njia za kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kisukari kama sehemu ya kuimarisha afya ya jamii, na kuwakumbusha wananchi kuchukua hatua muhimu ikiwamo kufanya mazoezi ya mara kwa mara walau kwa dakika 30 kwa siku kwa siku tano za wiki. 

Njia nyingine kwa mujibu wa Dkt.Chamba ni kula vyakula bora,kupunguza sukari,vyakula vyenye mafuta mengi na kuongeza mboga na matunda. 

Anashauri wananchi kujenga utamaduni wa kudhibiti uzito kwani uzito uliokithiri  huongeza hatari ya kupata kisukari na kusisitiza umhimu wa kupima  sukari mara kwa mara hasa kwa watu wenye  historia ya kisukari kwenye familia zao. 

 Msongo wa Mawazo ni moja ya visababishi vikubwa vya mtu kupata kisukari na daktri huyo Bingwa wa magonjwa ya ndani anashauri watu kupunguza  msongo wa mawazo . 

Anasema msongo wa Mawazo usipodhibitiwa  unaweza kuongeza kiwango cha sukari mwilini huku akiwaasa watu kuepuka  uvutaji sigara na pombe kupita kiasi . 

Anasema hayo yote yanachangia kuathiri afya ya kongosho na ongezeko la sukari na kwa wenye kisukari wanashauriwa kufuata ushauri wa madaktari kama tayari wana kisukari  na kushauri matumizi ya  dawa kwa wakati na kufuatilia kliniki. 

“Tunasisitiza ujumbe muhimu kupima ni kinga,kujua hali yako ya sukari ni hatua ya kwanza ya kulinda maisha yako”anasema. 

Amesma KCMC inaendelea kuwa mshirika wa karibu wa jamii katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza akiamini kwamba afya njema huanza na taarifa sahihi. 



  

Post a Comment

0 Comments