Wakazi wa Manispaa ya moshi wameiomba serikali kuchukua hatua dhidi ya wenye majengo yaliyochwaa muda mrefu.bila kuendelezwa
Wamedai kuwa baadhi ya majengo hayo yanaharibu madhali ya mji wa Moshi huku mengine yakigeuzwa kuwa maficho ya vibaka na wavuta Bangi.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti,wananchi hao wameitaka serikali kuwabaini wamiliki wa majengo hayo na kuwataka wayaendeleze .
Mmoja wa wananchi hao,Geness Kiwelu amesema baadhi ya .majengo hayo yanazaidi ya miaka 35 bila kuendelezwa hatua inayochangia kuuweka mji wa Moshi katika mazingira machafu.
Kiwelu ambaye amekuwa Diwani wa Manispaa ya moshi kwa vipindi vitatu,amesema mpango waliokuwa nao kama Baraza la Madiwani ilikuwa ni kujenga majengo marefu na si kukarabati majengo ya zamani .
Amewaomba madiwani na ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya moshi kuweka mkakati wa kuwafuatilia wamiliki wa majengo hayo ili wayaendeleze.
Kwa upande wake Stella Bundala alisema baadhi ya majengo hayo yamekuwa yakutumika kama madanguro pamoja na kuhifadhi mali za wizi huku baadhi ya vijana wakiyatumia kwa kufanya vitendo vya kiharifu.
Akizungumzia hali hiy,Mkuu wa Wilaya ya Moshi , Godfrey Mnzava ,amesema majengo hayo yanaharibu Taswira ya mji wa Moshi na kuwataka wamiliki wa majengo hayo kuweka mkakati wa kuyaendeleza pamoja na kuwafanyia usafi
Amesema baadhi ya watu wenye nia ovu wamekuwa wakiyatumia kama maficho ya wahalifu na baadhi kuyatumia kuficha mali za wizi na vitendo vingine viovu ikiwamo kuyatumia kama madanguro.
"Kwa mji wetu yapo majengo mengi ya aina hiyo na yanatumika vibaya na wananchi wasio na nia njema,ikiwemo kuhifadhi mali za wizi,vibaka wanajificha humo na mbaya zaidi kuna vitendo viovu kama ubakaji na ulawiti vinaendelea kwenye majengo hayo bila kusahau wengine wameyageuza kama gesti babu,"alisema
Alisema mkakati uliopo ni kuhakikisha watendaji wa serikali za mitaa na watendaji wa kata za manispaa ya moshi wanafanya sensa ya kujua idadi ya majengo hayo na kuhakikisha wamiliki wake wanapatikana


0 Comments