OFISI ZA CHAMA CHA MSINGI CHA USHIRIKA CHA KIRIMA BORO KAMA ZINAVYOONEKANA
WANACHAMA wa Chama cha msingi cha ushirika wa mazao cha Kirima Boro Amcos kilichopo wilaya ya moshi Vijijini,wamepaza sauti kwa mamlaka za uchunguzi kupiga kambi kwenye ofisi za chama hicho na kufanya uchuguzi juu ya madai ya viongozi wa muda wa chama hicho kudaiwa kuuza mashamba ya chama hicho kama ardhi ya ukoo maarufu kama vihamba kwa lugha ya kabila la Kichagga.
Wanadai kuwa
viongozi hao wamewauzia ardhi ya chama hicho watu mbalimbali wakiwamo
wanasiasa,wafanyabiashara wakubwa na watumishi wa umma jambo ambalo wanadai
haliendani na sera ya serikali katika mkakati wa kuendeleza ushirika nchini.
Timu yetu ya
uchunguzi iliyopiga kambi kwenye ushirika huo imeibua mengi ambayo bado
tunayafanyia uchunguzi ikiwamo majina ya waliouziwa ardhi hiyo Pamoja na
kuwatafuta mmoja baada ya mwingine ili kupata kauli zao juu ya kuuziwa ardhi ya
wanaushrika.
Kwa faida ya
wasomaji wetru,machi 21 mwaka 1967 vyama viwili vya msingi vya ushirika vya
Kimasio na Kirima Boro viliandika barua ya kuomba kununua shamba lililokuwa
likimiliwa na raia mmoja wa kigeni Tsoucas baada ya kubaini kuwa shamba hilo
haliendelezwi .
“Vyama
viwili vilivyotajwa hapo juu vinayo heshima kubwa kununua shamba hilo kwa
manufaa ya watu wote,baada ya uchunguzi mwingi kwa wahusikao na shamba hilo
ilionekana kuwa liko chini ya ulinzi wa manager wa Standard Bank”,inasema barua
hiyo na kuongeza.
“Baada ya
kumwona manager wa Bank alitoa dokezo kuwa shamba hilo ni ekari 450 na ni jumla
ya sh,600,000,kwa kifupi,shamba hilo halina mastawisho yeyote bali kuna vyumba
viwili tu(2),zaidi ya hapo tulikwisha julishwa kuwa alikuwa na deni
la Bank jumla ya sh,15,000”.
Kuambatana
na kima hicho cha sh,600,000,tunakuomba shamba hilo lichukuliwe kama bei hiyo
ni ya halali,tunatumai kuwa ombi letu hili litafikiriwa kwa
makini”,imehitimisha barua hiyo ambayo nakala yake timu yetu ya uchunguzi inayo
.
Kulingana na
uchunguzi wetu,Desemba 14 mwaka 2023 mwenyekiti wa Kijiji cha Boro,Laurent
Mushi kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho alimwandikia barua mkuu wa wilaya
ya Moshi akilalamikia mwenendo wa uongozi huo kuuza ardhi ya shamba la ushirika
kama vihamba akimuomba kuingilia kati
lalamiko hilo na kumuomba azuie mpango wa kugawa ardhi ya ushirika.
“Mh.Mkuu wa
wilaya baadhi ya wanakijiji wenye nia njema ya kudumisha amani wanakuomba
uingilie kati lalamiko hili na kuzuia mpango wa kugawa ardhi ya Ushirika inayosimamiwa
na Chama cha ushirika cha msingi cha Kirima Boro”.
Uratibu wa kumilikisha vipande vidogo vidogo vya ardhi usimame na badala yake eneo libaki kwa ajili ya Taasisi muhimu kwa umma mfano;Kituo cha Afya,Kituo cha Polsi Chuo cha ufundi n.k”.
“Wanakijiji
wamenieleza kuwa hofu yao ni kwamba mpango huu ukifanyika bila kuweka utaratibu
wa kisheria wa kumilikisha ardhi ambayo ni mali ya Ushirika,viashiria vya ugomvi
vinaweza kutokea katika shamba na kusababisha uvunjifu wa amani siyo tu kwa
wanachama wa chama cha Ushirika cha msingi bali pia kwa wakulima ambao baba zao
au mama zao ndio waliochangia fedha za kununua ardhi hiyo mwaka 1967 kutoka kwa
wamiliki wa kigeni na wamekuwa wakijiuliza maswali yafuatayo…….”
Pamoja na
kelele hizo kasi ya kuuzwa kwa ardhi ya ushirika inazidi kushika kasi,
Je ni kina
nani wanuza ardhi hiyo?
Je ni kina
nani wameuziwa ardhi hiyo?
Tunaomba
usikose kufuatalia Makala yetu ijayo ambayo itakuletea waliouza na waliouziwa

0 Comments