UJUE UGONJWA WA KUPOTEZA KUMBUKUMBU DEMENTIA,AMRCO YAJITOSA KAMPENI YA UPIMAJI WA AFYA KWA WAZEE

 

Mchungaji Rolland Syens kutoka Canada akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya AMRCO itakayokuwa mahususi kwa ajili ya  utoaji huduma ya upimaji wa afya kwa wazee wenyechangamoto ya ugonjwa wa Dementia eneo la Kindi Msasani wilaya ya moshi vijijini

 

Oktoba 27 mwaka huu shirika lisilo la kiserikali la  kumbukumbu ya Anderson  Memorial Rehabilitation(AMRCO )lilizindua ofisi yake ya kutoa huduma ya vipimo kwa wazee weye changamoto ya ugonjwa wa kusahau(Dementia)eneo la Kindi Msasani wilaya ya Moshi Vijijini. 

Lengo la kufunguliwa kwa ofisi hiyo ni kusogeza huduma karibu na kuwafikia wahitaji wengi ufunguzi huo ulienda sanjari na mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam na viongozi wa kijamii kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wazee wenye changamoto hiyo. 

Malengo mahususi ya mafunzo hayo ni kutoa huduma ya urekebishaji wa utunzaji kwa watu wanaoishi na ugonjwa wa kusahau . 

Makala hii fupi inaangazia mambo kadhaa ikiwamo kujua nini hasa maana ya Dementia.dalili za mwanzo za dementia na namna ya kukabiliana na tatizo hilo. 

DEMENTIA 

Huu ni  ugonjwa unaosababisha kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kufikiri na chanzo chake kinatajwa ni  kuharibika kwa seli za ubongo na visababishi vyake ni Pamoja na umri mkubwa.shinikizo la damu,ugonjwa wa moyo,kiharusi,kurithi na mabadiliko ya kemikali kwenye ubongo.  

NINI MAANA YA DEMENTIA? 

Demetia si ugonjwa mmoja bali ni Kundi mbalimbali zinazoathiri uwezo wa mtu kufikiri ,kukumbuka,kuwasiliana na kufanya shughuli za kila siku na mara nyingi huathiri wazee lakini si sehemu ya kawaida ya kuzeeka.

 

Dementia pia huathiri ubongo,Neuroni(seli za ubongo)zinazohusika na kumbukumbu ,lugha au tabia huanza kufa au kutofanyakazi ipasavyo,hali hii huanza polepole na kuendelea kuongezeka kadri muda unavyopita. 

Athari za Dementia kwa watu wenye umri mkubwa ni Pamoja na kupoteza kumbukumbu,kuchanganyikiwa,,kupoteza uwezo wa kujitawala,,mabadiliko ya tabia,ugumu wa kuwasiliana na watu. 

Kundi linaloathiriwa na Dementia kwa aslimia kubwa ni watu wenye umri wa miaka 65 na kuendelea,watu wenye historia ya familia ya ugonjwa huo,watu wenye shinikizo la damu,,watu wenye ugonjwa wa moyo na watu  wenye kiwango kidogo cha elimu.


Mkakati wa AMRCO ni kuhakikisha watu wenye changamoto hiyo wanafanyiwa uchunguzi wa mapema ili kubaini tatizo hatua ambayo inaweza itasaidia kudhibiti dalili na kupunguza athari zake. 

Hatua nyingine ni kuwawezesha kupata matibabu na matibabu ya dementia yanaweza kujumuisha,dawa,tiba ya kisaikolojia na mabadiliko ya mtindo wa maisha. 

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya,watu wenye tatizo la Dementia wanahitaji huduma ya kisaikolojia na usaidizi kutoka kwa familia na wataalamu wa afya. 

Kuhusu mabadiliko ya mtindo wa maisha wataalamu wa afya wanashauri mambo kadhaa yanayoweza kdhibiti dalili za Dmentia  ikiwamo  kufanya mazoezi, kula chakula bora, na kupunguza msongo wa mawazo . 

 Familia na walezi wanahitaji elimu kuhusu Dementia ili kutoa huduma bora kwa waathirika pamoja na kushirikiana na wataalamu wa afya kutokana na ukweli kwamba  watu wenye Dementia wanahitaji kushirikiana na wataalamu wa afya kama vile madaktari, wauguzi, na wataalamu wa kisaikolojia ili kupata huduma bora.

Graceanderson Fihavyango mratibu wa AMRCO akisoma taarifa fupi katika uzinduzi wa ofisi ya AMRCO hivi karibuni



 

Msomaji wetu endelea kutufuatilia kupitia kadama24blog kwani Makala yetu ijayo itaelezea Aina maarufu ya Dementia na je Deementia ni sawa na uzee wa kawaida?

 

 

Post a Comment

0 Comments