Kuna sintofahamu ya nani hasa anamiliki shamba la Sangiti huko Kibosho baada ya kuibuka watu wanaodai shamba hilo si mali ya ushirika bali ni mali ya wakulima mmoja mmoja hivyo wanayo haki ya kuuza kama vihamba.
Shamba hilo lilikua linamilikiwa na raia
wa kigeni na lilinunuliwa kupitia vyama viwili mwaka 1967 baada ya raia huyo wa
kuwa na deni benki ,wakulima walikatwa fedha za mauzo ya kahawa hadi pesa ikatoshea.
Kwa faida ya wasomaji wetu,machi 21
mwaka 1967 vyama viwili vya msingi vya ushirika vya Kimasio na Kirima Boro
viliandika barua ya kuomba kununua shamba lililokuwa likimiliwa na raia mmoja
wa kigeni Tsoucas baada ya kubaini kuwa shamba hilo haliendelezwi .
“Vyama viwili vilivyotajwa hapo juu
vinayo heshima kubwa kununua shamba hilo kwa manufaa ya watu wote,baada ya
uchunguzi mwingi kwa wahusikao na shamba hilo ilionekana kuwa liko chini ya
ulinzi wa manager wa Standard Bank”,inasema barua hiyo na kuongeza.
“Baada ya kumwona manager wa Bank
alitoa dokezo kuwa shamba hilo ni ekari 450 na ni jumla ya sh,600,000,kwa
kifupi,shamba hilo halina mastawisho yeyote bali kuna vyumba viwili
tu(2),zaidi ya hapo tulikwisha julishwa kuwa alikuwa na deni
la Bank jumla ya sh,15,000”.
Kuambatana na kima hicho cha
sh,600,000,tunakuomba shamba hilo lichukuliwe kama bei hiyo ni ya
halali,tunatumai kuwa ombi letu hili litafikiriwa kwa makini”,imehitimisha
barua hiyo ambayo nakala yake timu yetu ya uchunguzi inayo .
Katika mahojiano ya hivi karibuni
baadhi ya wananchi wanaoishi kirima wanasema wanaohusika na shamba hilo ni wale
tu ambao walikubali kukatwa fedha zao za mauzo ya kahawa na si wananchi wote
waliokatwa fedha kununua shamba hilo,
Wanajenga hoja kuwa wanaouza mashamba
hayo kwa watu ndiyo wenye sauti ya kuzungumzia uuzwaji wa mashamba hayo na si
kila mtu.
Hatua hii inakuja siku chache baada ya baadhi ya wanachama wa chama cha msingi cha ushirika cha Kirima Boro Amcos kupaza sauti kwa kuzitaka mamlaka za uchunguzi kuchunguza uuzwaji wa shamba hilo unaodaiwa kufanywa na Bodi ya usimamizi ya chama hicho.
Hali hiyo ilipelekea Tume ya maendeleo ya ushirika kupitia mrajis wa Ushirika nchini kutuma timu ya uchunguzi kuchunguza madai hayo.Inaelezwa kuwa wakulima walikuwa
wakikatwa senti saba kwa kila ratiri ya
kahawa waliyokuwa wakiuza chamani .
“Kila mtu anayomamlaka juu ya ardhi
yake na hao wanaolalamika kwamba ardhi inauzwa si wanufaika wa hayo mashamba
kwani hawakuwahi kukatwa fedha zao kwenye kahawa kununua mashamba hayo”
“Kuhusu mali zinazodaiwa kuuzwa tuhuma
hizi zi za kweli kwani hiyo trekta na jembe vyote vipo na unaweza ukaenda
chamani ukapiga picha”,anasema mmoja wa viongozi wa Bodi ya usimamizi.
Shamba hilo ambalo lilikuwa na ukubwa wa ekari 450 lilimegwa kwa ajili ya upanuzi wa Taasisi zikiwamo shule,makanisa,misikiti,kituo cha polisi na zanahati na kubakia ekari 142.
Baadae Kaskazini yenye vijiji vinne ,Kirima
Juu,Maua,Otaruni na Singa na kusini yeney vijiji viwili ambavyo ni Kirima kati na
Boro waliamua kugawa nusu kwa nusu kwa maana ya ekari 71 kila upande .
Kuhusu madai ya ujenzi wa ukumbi
unaoendelea kujengwa chamani hapo ,viongozi hao wanasema taratibu zote
zilizifuatwa na kupata baraka za wanachama .
Uongozi kwa kushirikiana na kamati ya
shamba ili kutoa ekari 2 na nusu kwa mabadirishano ikiwa ni mkakati wa kupata
pesa kufanikisha ujenzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Hashim Komu anasema
suala hilo lilipelekwa kwa wanachama ambao waliridhia na juni 20 waka jana
mkutano wa wananchama ulielekeza ifanyike tathimini ya gahraza za ujenzi wa
ukumbi huo.
Anasema Mei 29 mwaka huu taarifa ya tathimini iliwasilishwa kwenye mkutano wa wanachama na kupewa taarifa ya matokeo ya tathimini hiyo na kuridhia ujenzi uanze mara moja
Kuhusu ukaguzi wa hesabu za chama,uongozi huo unasema kila msimu shirika la ukaguzi wa hesabu za vyama vya ushirika la CAOSCO kila msimu limekuwa likikagua hesabu za chama hicho kwamba taarifa za ukaguzi zipo .




0 Comments