TARURA,TANROADS K'NJARO WAWASILISHA MPANGO WA MATENGENEZO NA UKARABATI WA BARABARA MWAKA WA FEDHA 2026/2027,NI KATIKA KIKAO CHA BODI YA BARABARA(ROAD BOARD) NA KAMATI YA USHAURI YA MKOA, RCC,

 

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Babu akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa(RCC)mwishoni wa wiki. 

Wakala wa Barabara za vijijini na mijini(Tarura) na wakala wa Barabara nchini (Tanroads)mkoa wa Kilimanjaro wamewasilisha taarifa ya mpango wa kazi kwa mwaka wa fedha 2026/2027  na kuomba fedha kutelekeza mpango huo . 

Wakala hizo ziliwasilisha mpango huo katika vikao vya Bodi ya Barabara(Road Board) na kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa(RCC)vilivyoketi kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya moshi na kufunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin babu. 

Meneja wa Tanroads mkoa wa Kilimanajro,Eng: Motta Kyando katika  mpango huo  wa kazi za mwaka wa fedha 2026/2027 ameomba  sh.Bilioni 281.693 kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa  barabara 

"Jumla ya sh,Bilioni 281.693 zimependekezwa kutumia katika miradi mbali mbali ya matengenezo,maendeleo,usimamizi na uendeshaji wa ofisi za mizani na uendeshaji wa mfumo wa usimamizi na matengenezo ya barabara na madaraja mkoani kilimanjaro kwa mwaka wa fedha 2026/2027"inasema sehemu ya Taarifa hiyo .

Mhandisi Kyando amesema katika taarifa hiyo kuwa kati ya fedha hizo ,sh,Bilioni 213.826 ni kutoka mfuko wa Barabara ,Bilioni 67.53 ni kutoka mfuko wa maendeleo (CF)na mfuko wa Barabara(RF),sh,Bilioni 1.918 ni kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji wa ofisi za mizani . 

Kwa Mujibu wa mhandisi Kyando ,sh,Milioni 145.231 ni kwa ajili ya uendeshaji wa mfumo wa usimamizi wa matengenezo ya barabara na madaraja (RAMS na BMST),usimamizi wa hifadhi ya barabara pamoja na usalama barabarani. 

Mpango huo utahusisha matengenezo ya kawaida barabara ya lami (KM. 294.52),matengenezo maalumu barabara za lami(km 236.00),matengenezo ya kinga ya madaraja 30,matengenezo makubwa ya daraja Moja . 

Wakala wa barabara mkoa wa kilimanjaro(Tanroads )unahudumia barabara zenye urefu wa KM 1,098.83 ikijumuisha KM. 292.74 za barabara kuu,KM.762.77 barabara za mkoa na KM. 43.32 barabara za wilaya.

Eng:Motta Kyando(wa pili kutoka kulia),meneja wa Wakala wa barabara nchini(Tanroads)mkoa wa Kilimanjaro.
 

Kulingana na Taarifa ya meneja huyo mkoa wa Kilimanjaro ,mtandao huo wa Barabara tajwa unajumuisha Barabara za lami zenye Jumla ya KM 536.00  za KM. 562.84 za changarawe. 

HALI YA BARABARA 

Kuhusu hali ya barabara kwa ujumla zinazohudumiwa na Tanroads Kilimanjaro  meneja huyo anasema hadi kufikia mwishoni mwa mwezi januari mwaka huu ni ya kuridhisha. 

Mhandshi Kyando anasema aslimia 55 ya barabara za lami zina hali nzuri ,aslimia 45 zipo katika hali ya wastani

Kwa upande wa Barabara za changarawe taarifa hiyo inaeleza kuwa aslimia 44.86 zina hali nzuri na aslimia 55.14 zipo katika hali ya wastani na kwamba mtandao wote wa Barabara unapitika vizuri kipindi chote cha mwaka . 

Mpango huo umeainisha changamoto ikiwamo  fedha kidogo  zinazotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na matengenezo ya barabara ikilinganishwa na mahitaji halisi hali ambayo imesababisha kupunguza baadhi ya mahitaji ili kuendana na bajeti iliyopo.

                                               Wajumbe

 

TARURA K'NJARO YAOMBA BIL.36.685,908,351,127 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO. 

Kwa upande wa wakala wa Barabara za vijijini na mjini mkoa wa Kilimanjaro(Tarura),imewasilisha mpango wa matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2026/2027 . 

Akiwasilisha mpango huo ,meneja wa  Tarura mkoa wa Kilimanjaro,,Mhandisi  Juma Wambura amesema wakala imeomba jumla ya sh,,Bilioni 36,686,908,351.127 kutoka vyanzo vyake vitatu .

Vyanzo hivyo ni pamoja na mfuko wa Barabara (Road Fund Board )kiasi cha sh,Bilioni 17,453,933,351.09,serikali kuu(CF)majimbo kiasi Cha sh,Bilioni 5,serikali kuu tozo ya mafuta(Fuel Levy)sh,Bilioni 24,231,975,000.00.


Eng:Juma Wambura ,Meneja wa Tarura mkoa wa Kilimanjaro. 

Tarura mkoa wa Kilimanjaro inahudumia mtandao wa Barabara wenye urefu wa KM. 4685,483,madaraja 1129 ,makalvati ya saizi mbalimbali 5,070 katika wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro . 

Kwa Mujibu wa Mhandisi Wambura ,kati ya hizo KM 237,090 ni barabara za lami za zege ,KM 1,722,927 ni barabara za changarawe na KM 2,725,459 ni za udongo. 

Kuhusu hali ya barabara mhandisi Wambura anasema KM. 900,805 (19%)zipo katika hali nzuri,KM 2,474,495(53%) zipo katika hali ya kkuridhisha na KM. 1,310 ,183 (28%)zipo katika hali mbaya . 

Wambura amesema katika taarifa yake kwa wajumbe wa Bodi ya barabara kuwa jumla ya KM. 3,375.30 sawa na aslimia 71.6 hupitika wakati wote wa mwaka na KM. 2,310,183 sawa na aslimia 24.4 hupitika kwa shida hasa wakati wa mvua .


Wajumbe kutoka vyama vya siasa

"Katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2026/2027 ya sh,Bilioni 36.6 wakala imepanga kutengeneza barabara za lami . 16.77,barabara za changarawe km. 343.23,matengenezo sehemu korofi  na ya kawaida km. 950 .87,makalvati 44,madaraja 9,mitaro mita 830 na taa za barabarani 180",inasema Taarifa hiyo.

Tarura pia imeanisha changamoto inazokabiliana nazo katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwamo bajeti ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi ya ujenzi na matengenezo katika mkoa. 

Changamoto nyingine ni uharibifu wa miundombinu ikiwamo wizi wa alama za barabarani ,kingo za madaraja,utupaji wa taka kwenye mifereji ya maji na ukataji wa Barabara usiofuata taratibu. 


Wajumbe kamati ya ulinzi na usalama.

"Wakala wa barabara za vijijini na mijini (Tarura)mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na ofisi  ya mkuu wa mkoa ,mamlaka za serikali za mitaa (Tanroads ,Ruwasa,nk)  tutaendelea  kuhudumia mtandao wetu hasa maeneo ya vipaumbele yenye huduma za kijamii (masoko ,afya  na elimu)" 

"Maeneo ya uzalishaji wa Kilimo,ufugaji na viwanda ili kuhakikisha maeneo hayo yanafikika msimu mzima wa mwaka "inahitimisha taarifa hiyo .



Post a Comment

0 Comments