Mkuu wa wilaya ya Chato,Louis Bura,ameiangiza Halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita kutunga sheria ndogo zitakazowabana wazazi wanaoshindwa kuchangia chakula cha watoto wao shuleni.
Agizo hilo amelitoa Februari 11,mwaka huu wakati wa kilele cha maadhimisho ya.siku ya Wanawake na wasichana katika sayansi yaliyofanyika kwenye shule ya msingi ya Miembeni wilayani Chato.
Amesema ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha anachangia fedha kwa ajili ya chakula cha watoto shuleni huku akionya hatua zaidi zichukuliwe kwa wataoshindwa kuchangia fedha za chakula.
Amesema mtoto ambaye hapati chakula cha mchana shuleni hawezi kuwa na usikivu mzuri wakati wa masomo darasani .
"Naomba niwaulize mtoto wako akiwa nyumbani mchana hatakula chakula? ,ni wakati mwafaka sasa Halmashauri zitunge kanuni kuhakikisha kila mzazi anachangia chakula cha watoto shuleni ",Alisema.
Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Maendeleo ya vijana na fursa kwa wanawake Tanzania maadhimisho yanayolenga kuhamasisha maendeleo ya elimu ya sayansi na ushiriki wa wanawake na wasichana katika ujenzi wa maarifa na ubunifu .
Katika
Taarifa yake kwa mgeni rasmi ,Mkurugenzi wa Shirika hilo ,Febronia Ignus
Massawe alitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt.
Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake thabiti na wa maono uliothibitisha kuwa
sayansi inawezekana Tanzania.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Maendeleo ya vijana na fursa kwa wanawake Tanzania,Febronia Ignus Massawe(kushoto)akiongozana na mkuu wa wilaya ya Chato,Louis Bura kuelekea viwanja wa shule ya msingi miembeni kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya wanawawake na wasichana katika sayansi.
Amesema kupitia Serikali yake, kumekuwa na maboresho makubwa katika sekta ya elimu, ikiwemo mabadiliko na uboreshaji wa sera ya elimu, uimarishaji wa miundombinu ya shule, upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia, pamoja na kuhimiza ushiriki wa wasichana katika masomo ya sayansi, teknolojia na ubunifu.
"Ndugu mgeni rasmi hatua hizi zimeongeza fursa, matumaini na imani kwa kizazi cha sasa na kijacho",amesema .
"Mheshimiwa Mgeni Rasmi,lengo la maadhimisho haya ni kuwahamasisha wasichana na wanawake kupenda, kusoma na kushiriki kikamilifu katika masomo ya sayansi na hisabati, ambayo ni msingi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi".
"
Tunaamini kuwa kumuandaa msichana katika sayansi ni kuwekeza katika maendeleo
endelevu ya taifa.katika kuunga mkono dhamira hii, leo tumetekeleza shughuli
mbalimbali ikiwemo upandaji wa miti kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi"
"Mengine ni uchangiaji wa chakula kwa wanafunzi wa Darasa la Saba, ili kuongeza motisha na kuboresha mazingira ya kujifunzia",
Kwa Mujibu wa mkurugenzi huyo amesema bado zipo changamoto zinazokwamisha ushiriki wa wasichana katika masomo ya sayansi, zikiwemo mitazamo hasi na changamoto za kiuchumi.
"Kupitia hotuba hii, tunaomba ushirikiano wa viongozi, walimu na wazazi kuendelea kuondoa vikwazo hivyo na kutoa fursa sawa za elimu kwa watoto wote bila ubaguzi wa kijinsia",amesema
Amesema kwa upande wao kama Shirika la Maendeleo ya Vijana na Fursa kwa Wanawake Tanzania, wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuibua vipaji, kutoa elimu na kuendeleza programu zitakazowawezesha vijana na wanawake kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
"Mwisho, tunatoa shukrani kwa uongozi wa shule, walimu, wazazi na wadau wote waliofanikisha tukio hili,ttunawahimiza wanafunzi wetu, hasa wasichana, kujiamini, kusoma kwa bidii na kutambua kuwa ndoto zao katika sayansi zinawezekana",alihitimisha hotuba yake









0 Comments