MWANGA-KILIMANAJRO
MGOMBEA
ubunge jimbo la Mwanga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Ngwaru
Jumanne Maghembe, amezindua rasmi kampeni za ubunge na kuahidi kushughulikia
kero kubwa zinazowakabili wananchi wa jimbo la Mwanga ikiwamo tatizo kubwa la
uvamizi wa Tembo ambao wamekuwa tishio kwa usalama na mali za wananchi hao.
Dkt.Ngwaru
ambaye aliteuliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa baada ya kupata
ushindi mkubwa kwenye kura za maoni wa kura 4,108 akimbwaga aliyekuwa mbunge wa
Jimbo hilo,Wakili Joseph Tadhayo aliyeambulia kura 1,689,alizindua kampeni zake
kwenye Tarafa ya Usangi.
Katika
uinduzi huo,Dkt.Ngwaru alisema atashirikiana na TAWA kuhakikisha k inajengwa
kituo cha kukabiliana na Tembo eneo la Jipendea ambako ni moja ya maeneo ambayo
yamekuwa yakikabiliwa na uvamizi wa tembo kwenye makazi ya watu pamoja na
kuharibu mazao yao.
“Tutahakikisha
tuna fungua ofisi pale Jipendea ili wenzetu wa Tarafa ya Jipendea, Kwakoa,
Mgagao, Toroha na Kirya wasiendelee kupata shida na hili tutashirikiana
na wenzetu wa TAWA ili tuwe na ofisi Jipendea yenye vifaa vyote vya kukabiliana
na tembo pamoja na askari wa kutosha“,alisema.
Kuhusu tatizo
la maji katika baadhi ya maeneo jimboni humo,Dkt.Ngwaru aliahidi yeye kwa
kushirikina na madiwani watakaochaguliwa kushughulikia kero hiyo ya maji ambayo
imkuwa ni ya muda mrefu.
Alipongeza
hatua ya serikali kuufufua mradi mkubwa wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe ambao
ulikuwa ni wa kusuasua hadi hapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoamua kutoa
pesa kuuendeleza.
“Mimi
nimekuwa mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa miaka
minane, nchi yetu ni tofauti kabisa na nchi nyingine ndani ya Jumuiya,ni
bahati nzuri sana sisi tunaishi kwa Amani na Uhuru pamoja na mipango mizuri ya
kuwaletea maendeleo wananchi”alisema na kuongeza.
“Hii ni
kutokana na kuwa na viognozi wachapa kazi na makini chini ya Jemedali wetu Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais ni mfuatliaji mzuri wa miradi ya maendeleo
ukiwamo mradi wa maji wa Mwanga-Same hadi Korogwe.”
“Mradi huu
ulioanza mwaka 2014 ulisuasua sana hadi Rais wetu alipoamua kutoa pesa ili
mradi uendelee na sasa mradi huo umekamilika haya yote ni kwa sababu ya kuwa na
viongozi wachapa kazi”,alisema.
Kwenye suala
la Afya, Dk.Ngwaru alisema atahakikisha vituo vyote vya afya pamoja na zahanati
vinajengwa ili kuwaondoea kero wananchi wa jimbo la Mwanga na kuahidi
kutoa fotari 5,000 na mifuko 100 ya saruji kwa kila zanahati itakayojengwa.
Alisema hadi
sasa serikali imeweza kujenga majengo 10 kwenye Hospital mpya ya Wilaya
ya Mwanga na kwa sasa bado majengo 18 yatajengwa ikiwamo chumba cha upasuaji
pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya Chomvu kitakachokuwa na jengo la huduma ya
mama na mtoto.
Akizungumzia
changamoto ya miundombinu ya barabara alisema mpango wa serikali ni kujenga
barabara kwa kiwango cha lami kwa baadhi ya barabara ambazo ni mhimu katika shughuli
za uzalishaji mali.
Aliahidi pia
ujenzi na ukarabati wa minada ya ng’ombe ya Kileo na Mgagao lengo ni kuifanya
minada hiyo kuwa kitovu kikubwa kwa Kanda wa kaskazini huku akiahidi
kushughulikia suala la umeme kwenye vitongoji sita ambavyo havina umeme.
Dkt.Ngwaru aliahidi kushughulikia ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji ikiwamo ujenzi wa soko la mazao la Kituli.
.jpg)
.jpg)





0 Comments