MWANGA-KILIMANAJRO
MAKUNDI ya Tembo ambayo yamekuwa yakivuka kutoka Hifadhi ya Taifa ya Tsavo West nchini Kenya na kuingia nchini hasa wilaya ya Mwanga, yamekuwa tishio kwa usalama wa maisha na mali za wananchi.
Tembo hao wamekuwa wakivamia na kuharibu mazao ya wananchi pamoja na kuhasababisha vifo vya wananchi na kufifisha jitihada za wananchi kuendelea na shughuli za kilimo.
Ni kutokana na hali hiyo, wananchi hao wameendelea kupaza sauti kuomba msaada kwa serikali kuchukua hatua za kukabiliana na makundi hayo ya Tembo.
Katika kuhakikisha kuwa tatizo hilo linatafutiwa ufumbuzi wa kutosha, Dkt.Ngwaru Jumanne Maghembe ambaye ni mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la Mwanga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),ameahidi wananchi kushughulikia kero hiyo kubwa.
Maeneo ambayo yamekuwa yakilengwa na Tembo hao wanaopitia hifadhi ya Taofa ya Mkomazi kwa upande wa Tanzania ni Toroha, Kivisini, Kwakoa, Kileo, Kirya na Jipe.
Dkt.Ngwaru aliteuliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa baada ya kupata ushindi mkubwa kwenye kura za maoni wa kura 4,108 akimbwaga aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo,Wakili Joseph Tadhayo aliyeambulia kura 1,689,alizindua kampeni zake kwenye Tarafa ya Usangi.
Katika uinduzi huo,Dkt.Ngwaru alisema atashirikiana na TAWA kuhakikisha kinajengwa kituo cha kukabiliana na Tembo eneo la tarafa ya Jipendea ambako ni moja ya maeneo ambayo yamekuwa yakikabiliwa na uvamizi wa tembo kwenye makazi ya watu pamoja na kuharibu mazao yao.
“Tutahakikisha tuna fungua ofisi pale Jipendea ili wenzetu wa Tarafa ya Jipendea, Kwakoa, Mgagao, Toroha na Kirya wasiendelee kupata shida na hili tutashirikiana na wenzetu wa TAWA ili tuwe na ofisi Jipendea yenye vifaa vyote vya kukabiliana na tembo pamoja na askari wa kutosha“,alisema.







0 Comments