NITAENDELEZA WALIPOISHIA WATANGULIZI WANGU,ASEMA DKT.NGWARU MAGHEMBE

MWANGA-KILIMANJARO

MBUNGE wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na mgombea ubunge jimbo la mwanga kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi(CCM),DKT.Gwaru Jumanne Maghembe,ameahidi kuendeleza pale walipoishia watangulizi wake.

Dkt.Gwaru ametoa kauli hiyo wilayani mwanga mkoani Kilimanjaro muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya uteuzi kuwania kiti cha ubunge kwenye jimbo hilo kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la mwanga.

Alianza kumshukuru waziri Mkuu mstaafu na Baba wa Mwanga,marehemu Cleopa David Msuya ambaye alikuwa mbunge wa kwanza wa jimbo la mwanga.

Pili akamshukuru Profesa Jumanne Maghembe ambaye pia ni Baba yake mzazi aliyehudumu katika jimbo hilo kwa muda wa miaka 25.

Dkt.Ngwaru pia alimshukuru mtangulizi wake wakili Msomi Joseph Thadayo na kueleza kuwa atashughulikia changamoto ya umeme kwa baadhi ya vijiji ambavyo havina nishati ya umeme ndani ya jimbo hilo.

Pia aliahidi kushughulikia changamoto ya ukosefu wa vyumba vya Madarasa kwa baadhi ya shule za msingi jimboni humo.

Akizungumza na umati wa wanachama wa chama hicho waliofulika nje ya jengo jipya la Halmashauri ya wilaya ya Mwanga, Dkt.Ngwaru alisema uchaguzi ndani ya chama umemalizika na sasa nguvu inaelekezwa katika kuhakikisha jimbo hilo linabaki mikononi mwa CCM kwa chama hicho kupata ushindi wa kishindo.

Kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho,Dk. Ngwaru Jumanne Maghembe aliibuka mshindi kwa kupata  kura   4,108 huku akimuacha kwa mbali mshindnani wake na aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Joseph Anania Thadayo,aliyepata kura 1,689, huku ndugu Ramadhani Ally Mahuna akifuatia kwa kupata kura 720.




Post a Comment

0 Comments