MOSHI-KILIMANJARO.
PAZIA la uchukuaji wa fomu kuwania nafasi ya ubunge katika majimbo ya uchaguzi nchini limefunguliwa rasmi ambako katika jimbo la moshi Mjini,makada wawili maarufu wa chama hicho wameuangana kuhakikisha jimbo hilo linaendelea kubaki kuwa mali ya chama cha mapinduzi(CCM)katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.
Priscus Tarimo mbunge aliyemaliza muda wake(ccm)ambaye Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Tiafa iliengua jina lake licha ya kuongoza kura za maoni,ameungana na Ibrahim Shayo mfanyabiashara maarufu mjini moshi aliyeteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera ya CCM.
Kuungana kwa makada hawa wawili kumeondoa minong’ono iliyokuwa imesambaaa Mjini moshi kuwa huenda Priscus akajitenga na mteule huyu wa CCM lakini hii ndiyo CCM chama kilichojikita mizizi takribani miaka 50 sasa.
Mara baada ya Ibrahim Shayo maarufu kwa jina la Ibra Line kuchukua fomu kwenye ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi,Priscus aliweka bayana kuwa ndani ya chama cha mapinduzi hakuna kununiana pale ambako chama kinapoteua mgombea na kazi iliyobaki sasa ni kuhakikisha chama kinalipigania jimbo hilo liendelee kubaki mikononi mwa CCM.
Priscus alisema na hapa namnukuu”hii ndiyo cc,hatununiani na tutahakikisha kura zote za rais,wabunge na madiwani zinajaa na umoja wetu ndiyo ushindi wetu”,mwisho wa kunukuu.
Ibrahim Shayo alikuwa mwenye furaha wakati wa uchukuaji wa fomu na hakuficha hisia zake alipozungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la moshi Mjini Sifael Kulanga.
“Hakuna siku nimekuwa na furaha kama siku ya leo,napenda kumshukuru mwenyekiti wangu wa CCM taifa na Kamati yake kwa kuniamini na kuniteua kugombea ubunge jimbo la moshi Mjini wanamoshi wanamatarajio makubwa sana kutoka kwangu sasa niko tayari kushirikiana nao na kuleta maendeleo katika mji wetu”,alisema.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la moshi Mjini ,Sifael Kulanga aliwaambia waandishi wa habari kuwa mpaka sasa ni vyama tisa tu kati ya 18 vyenye usajili wa kudumu wanachama wake wamechukua fomu kwa ajili ya kuwania kiti cha ubunge katika uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani hapo oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Moshi Mjini,Sifael Kulanga,vyama hivyo ni pamoja na chama cha mapinduzi(CCM),vingine ni chama cha wananchi(CUF),Tanzania Labour Paty(TLP),Chama cha SAU,MAKINI,CCK,AAFP,NRA pamoja na CHAUMA.
Mchakato wa uchukuaji fomu
za kuwania kiti cha ubunge ni wa siku tatu kuanzia Tarehe 25 hadi Agosti 27
ambayo ni siku ya urejeshaji wa fomu kabla ya kuanza kwa kampeni rasmi hapo
Agosti 28 zitakazohitimishwa siku moja kabla ya zoezi la upigaji kura.







0 Comments