ALHAJ IBRAHIM SHAYO:MKINICHAGUA KUWA MBUNGE WETU NITAHAKIKISHA TUNAFUFUA KIWANDA CHA MAGUNIA

  
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Moshi Mjini,Faraj Kibaya Swai(Kushoto)akimnadi kwa wananchi wa kata ya Kaloleni mgombea ubunge kupitia chama hicho jimbo la moshi mjini,Alhaj Ibrahim Shayo. 

                           MOSHI-KILIMANJARO

MGOMBEA wa kiti cha ubunge jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM),Alhaj Ibrahim Shayo,amewaahidi wananchi wa moshi mjini kuwa endapo atachagulikuwa kuwa mbunge wao katika uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani Oktoba 29 mwaka huu,atashirikiana na serikali kuhakikisha kiwanda cha magunia cha mjini moshi kinafufuliwa na kutoa ajira kwa wananchi.

Ahadi hiyo ameitoa kwa nyakati tofauti katika kata za Mfumuni na Kaloleni wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM kwenye mikutano ya kampeni za uchaguzi zinazoendelea mjini moshi.

Alisema kiwanda hicho cha magunia|(Tanzania Bag Corporation)kilichofunguliwa rasmi machi 31 mwaka 1970 na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere,ni moja ya viwanda vilivyokuwa vikitoa ajira kubwa kwa wananchi wa moshi.

Kiwanda hicho kilitisha uzalishaji mwaka 1999 na kubinafsishwa kwa kampuni moja chini ya utawala wa awamu ya tatu wa marehemu Benjamin Willium Mkapa na tangu wakati huo kilibaki kuwa gofu.

Mbali na kiwanda hicho,mgombea huyo pia aliahidi endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la moshi mjini,atafuatilia na kujua ni sababu gani ilisababisha viwanda vingi vilivyokuwa vikitoa ajira kwa wananchi wa moshi vimekufa.

Mgombea ubunge jimbo la Moshi mjini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM),Alhaj Ibrahim Shayo(Pichani)akizungumza kwenye mkutano wa kampeni kata ya Kaloleni.

Miongoni mwa viwanda atakavyovifutilia ni Pamoja na kiwanda cha Ngozi cha Moshi ambacho kwa muda mrefu kimesitisha huduma zake na,Kibo Match,Kibo Peper ni moja ya viwanda vilivyokuwa vikitoa ajira kubwa kwa wananchi wa moshi,hivi vyote havizalishi tena.

Aliwataka wananchi wa |Jimbo la Moshi mjini kufanya uamuzi oktoba 29 kwa kumpigia kura za kishindo mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM),Rais Dtk.Samia Suluhu Hassan,yeye kwa nafasi ya ubunge na madiwani kupitia CCM.

Alisema kwa kufanya hivyo itampa nguvu yeye kama mbunge kupeleka kilio cha wanamoshi kwa mheshimiwa Rais ili aweze kuwapelekea fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

“Mheshimiwa Rais wetu amefanya mambo mengi mazuri katika mji wetu wa Moshi,ametuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospital yetu ya wilaya inayojengwa kata ya Ng’ambo,ametuletea fedha zikakarabati shule zetu kongwe za sekondari,leo ukienda Mawenzi Sekondari madhari ya shule hiyo ni kama makazi ya mtu binafsi”,alisema. 

Akiwa kata ya Kaloleni,Alhaji Ibrahim Shayo aliwaeleza wananchi wa moshi kuwa,yeye ni mtoto anayetoka familia maskini kwani baba yake mzazi alikuwa akiuza machungwa stendi ya mabasi.

“Najua shida za wananchi wa moshi mjini,mimi natoka familia maskini,baba yangu alikuwa akiuza machungwa stendi,kwa hiyo shida zenu naifahamu sana,naishi moshi mjini,nafanyabiasharazangu za mafuta na mabasi  moshi mjini”,alisema

Alisema wabunge wengi wanashindwa kuwatumikia wapiga kura wao kutokana na kutokujua wajibu wao kama wabunge hivyo akasema yeye haendi bungeni kujifunza wajibu wa mbunge kwa wapiga kura wake.

Mgombea huyo wa kiti cha ubunge pia ameeendelea kuzungumzia kero ya tka mjini moshi zinazochangiwa na uhaba wa magari ya kuzoa taka ambako ameahidi  kuwa akichagulwa kuwa mbunge atakwenda kushirikiana na madiwani kuhakikisha yanannunuliwa magari zaidi  kwa ajili ya kuzoa taka.

 

Alisema mji wa moshi ambao unasifika kwa usafi kwa sasa unakabiliwa na mrundikano wa taka unaosababishwa na uhaba wa magari ya kuzoa taka hali inayosababisha baadhi ya maeneo kuwa na mrundikano wa taka.

“Ndugu zangu wananchi niseme wazi kuwa mji wetu kwa sasa unachangamoto ya magari ya kuzoa taka,sasa mkinichagua kuwa mbunge wenu nakwenda kushirikiana na madiwani wenzangu ili tuongeze magari ya kuzoa taka ili kuuweka mji wetu katika hali ya usafi”,alisema. 

 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi(CCM)moshi mjini,Faraj Kibaya Swai wa kwanza kutoka kushoto akifurahia jambo na mgombea ubunge jimbo la moshi mjini wa pili kutoka kushoto,Alhaj Ibrahim Shayo,anayefuatia ni katibu wa CCM Moshi Mjini,Frida Kaaya na mgombea udiwani kata ya Kaloleni,Nassib Maliki wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Kaloleni

 

Post a Comment

0 Comments