PASUA-MOSHI.
MGOMBEA wa
Kiti cha Ubunge Jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), Ibrahim Shayo amewaomba wananchi wa Kata ya Pasua kumchagua kuwa
mbunge wao ili akapiganie kata hiyo kuwa na Zahanati na kuondokana na usumbufu
wa kutebea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya.
Ametoa hadi
hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la kwa Mberere Matindigani
katika kata ya Pasua iikiwa ni mfululizo wa mikutano ya kampeni kuelekea
uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika oktoba 29 mwaka huu.
Alisema kwa
muda mrefu wananchi wa kata ya paua wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya
muda mrefu ya kutokuwa na Zahanati na kueleza kuwa ndani ya siku 60 za ubunge
wake atahakikisha kuwa anashirkiana na madiwani kupata zahanati.
Shayo
maarufu kwa jina la kaka wa jimbo, alisema katika kipindi cha miaka minne ya serikali
ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeipatia manispaa ya
moshi zaidi ya shilingi Bilioni 277.9.
Alisema fedha hizo zimeelekezwa kwenye sekta ya afya ambako zimesaidia pia ujenzi wa hopsital ya wilaya ,sekta ya elimu ikiwamo ukarabati wa shule kongwe za sekondari, Old Moshi, Mawenzi Sekondari na Moshi Tech.
Katika hatua nyingine,mgombea huyo alisema kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Moshi mjini,atashirikiana na madiwani watakaounda Baraza la Madiwani Manispaa ya Moshi kuhakikisha yanannunuliwa magari zaidi kwa ajili ya kuzoa taka.
Alisema mji wa Moshi ambao unasifika kwa usafi kwa sasa
unakabiliwa na mrundikano wa taka unaosababishwa na uhaba wa magari ya kuzoa
taka hali inayosababisha baadhi ya maeneo kuwa na mrundikano wa taka.
“Ndugu zangu wananchi niseme wazi kuwa mji wetu kwa sasa
unachangamoto ya magari ya kuzoa taka,sasa mkinichagua kuwa mbunge wenu
nakwenda kushirikiana na madiwani wenzangu ili tuongeze magari ya kuzoa taka
ili kuuweka mji wetu katika hali ya usafi”,alisema.
Mgombea huyo kwa kiti cha ubunge pia alizungumzia msongamano wa
magari kwenye barabara ya Double Road hasa eneo la Mbuyuni ambayo imekuwa
kero hasa nyakati za jioni na kuahidi kuweka mkakati wa kuweka Taa za kuongoza
magari.
Alizungumzia pia suala la miundombinu ya barabara na kuahidi
kushughulikia baadhi ya maeneo yenye changamoto hiyo na kuongeza kuwa atakwenda
bungeni kujenga hoja ili serikali iongeze fedha kwenye miundombinu ya barabara
katika mji wa moshi.
“Mheshimiwa Rais wetu amefanya mambo mengi mazuri katika mji
wetu wa Moshi,ametuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospital yetu ya wilaya
inayojengwa kata ya Ng’ambo,ametuletea fedha zikakarabati shule zetu kongwe za
sekondari,leo ukienda Mawenzi Sekondari madhari ya shule hiyo ni kama makazi ya
mtu binafsi”,alisema.
Aliwataka wanamoshi kumpa kura nyingi Rais Dkt.Samia Suluhu
Hassan ili nae apate nguvu ya kwenda kumlilia shida za wanamoshi pale
atakapochaguliwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo wa Oktoba 29
mwaka huu
Mkutano huo pia ulitumika kumnadi mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Pasua Barreh Farrah mmoja wa wagombea udiwani vijana alieahidi kushirikiana na madiwani wenzake kuleta maendeleo kwa wananchi wa Pasua.
Mkutano huo wa kampeni pia ulihudhuliwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Moshi mjini,Faraj Kibaya Swai,Katibu wa CCM Moshi Mjini,Frida Kaaya,Katibu wa Mwenezi wa CCM Moshi Mjini,Athuman Mfutu pamoja na katibu wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro.









0 Comments