MOSHI-KILIMANJARO
MGOMBEA wa
kiti cha Ubunge kupitia Chama Cha mapinduzi(CCM),mfanyabiashara tajiri ,Ibrahim
Shayo maarufu kwa jina la Ibra Line,amesema endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa
jimbo la moshi mjini,atashirikiana na madiwani watakaounda Baraza la madiwani
Manispaa ya Moshi kuhakikisha yanannunuliwa magari zaidi kwa ajili ya kuzoa taka.
Shayo mmoja wa wafanyabiashara maarufu katika sekta ya mafuta na usafrishaji ,ametoa ahadi hiyo katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Mfumuni eneo ya NHC kuelekea uchanguzi Mkuu wa Rais,wabuge na madiwani utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Alisema mji
wa moshi ambao unasifika kwa usafi kwa sasa unakabiliwa na mrundikano wa taka
unaosababishwa na uhaba wa magari ya kuzoa taka hali inayosababisha baadhi ya
maeneo kuwa na mrundikano wa taka.
“Ndugu zangu
wananchi niseme wazi kuwa mji wetu kwa sasa unachangamoto ya magari ya kuzoa
taka,sasa mkinichagua kuwa mbunge wenu nakwenda kushirikiana na madiwani
wenzangu ili tuongeze magari ya kuzoa taka ili kuuweka mji wetu katika hali ya
usafi”,alisema.
Mgombea huyo
kwa kiti cha ubunge pia alizungumzia msongamano wa magari kwenye barabara ya
Double Road hasa eneo la Mbuyuni ambayo
imekuwa kero hasa nyakati za jioni na kuahidi kuweka mkakati wa kuweka Taa za
kuongoza magari.
Alizungumzia
pia suala la miundombinu ya barabara na kuahidi kushughulikia baadhi ya maeneo
yenye changamoto hiyo na kuongeza kuwa atakwenda bungeni kujenga hoja ili
serikali iongeze fedha kwenye miundombinu ya barabara katika mji wa moshi.
“Mheshimiwa
Rais wetu amefanya mambo mengi mazuri katika mji wetu wa Moshi,ametuletea fedha
kwa ajili ya ujenzi wa Hospital yetu ya wilaya inayojengwa kata ya Ng’ambo,ametuletea
fedha zikakarabati shule zetu kongwe za sekondari,leo ukienda Mawenzi Sekondari
madhari ya shule hiyo ni kama makazi ya mtu binafsi”,alisema.
Aliwataka wanamoshi
kumpa kura nyingi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili nae apate nguvu ya kwenda
kumlilia shida za wanamoshi pale atakapochaguliwa kupeperusha bendera ya CCM
katika uchaguzi huo wa Oktoba 29 mwaka huu
Mkutano huo
pia ulitumika kumnadi mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Mfumuni Stuart Nathaniel
Nkini ambaye pia amekuwa Naibu Meya wa manispaa ya Moshi kwa miaka minne na kwa
sasa anasubiria kupigiwa kura za ndiyo au hapana baada ya kutopata mpinzani
kwenye kata yake.
Kwa upande
wake kada mpya wa CCM na ambaye alikuwa mbunge wa viti maalumu(Chadema)katika
Bunge lililopita,Felista Njau amemwagia sifa kem kem Ibrahim Shayo kwa mema
ambayo amekuwa akiyafanya mara kwa mara akiwa si mbunge.
“Wema
unajibiwa kwa wema,tuingieni mitaani tukatafute kura kwa ajili ya Ibra
Line,ametufanyia mema hata hajawa mbunge,je akiwa mbunge atatufanyia mema
mangapi”,alisema mwanamama huyo ambaye alikuwa mmoja wa watia nia ndani ya CCM
jimbo la Moshi Vijijini na kushika nafasi ya tatu.
Mkutano huo
wa kampeni pia ulihudhuliwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Moshi
mjini,Faraj Kibaya Swai,Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kilimanjaro,Elizabert Maro
Minde,makada mbali mbali na baadhi ya wagombea wa nafasi za udiwani na mgombea
huyo anaendelea na kampeni zake kwenye kata za Msaranga,Mawenzi na kwingineko.









0 Comments