MOSHI-KILIMANJARO
HALMASHAURI
ya manispaa ya moshi imepokea shilingi Bilioni 22.956 kwa ajili ya uboreshaji
wa miundombinu ya Barabara na mifereji ya maji ya mvua katika kata nane kati ya
kata 21 za manispaa ya moshi.
Fedha hizo
zitatumika katika ujenzi wa kilometa
13.2 za Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Ruwaichi hadi Njoro yenye
urefu wa kilomita 6.9,barabara ya pepsi
yenye urefu wa kilometa 1.25 na
Shirimatunda hadi magereza yenye urefu wakilometa 5.1.
Aidha chini
ya mradu huo kutakwepo na ujenzi wa mitaro ya kutiririsha maji ya mvua ukiwamo
mtaro kutoka Chuo Kikuu cha ushirika
kupitia, Key’s Hotel hadi Moshi Pazuri wenye urefu wa kilometa 2.0 na mtaro wa Kibong’oto wenye urefu wa kilometa 1.9..
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwenye hafla fupi ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miradi hiyo ya TACTIC kwa manispaa ya Moshi,mhandisi Emmanuel Manyanga kwa niaba ya mtendaji mkuu wa Tarura,alisema kuwa mradi huo unatekelezwa na serikali kuu kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Alisema
mradi huo utatekelezwa na mkandarasi ya M/S Hari Singh and Sons itakayotekeleza
kwa ushirikiano na kampuni ya ukandarasi ya Peritus Exim Private Limited na hii
ni awamu ya pili ya utekelezaji wa miradi hiyo ambako miji 15 ya kundi hilo la
pili ikiwamo manispaa ya moshi tayari wamekamilisha taratibu za wazabuni.
“Mradi wa
TACTIC ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na serikali kuu kupitia mkopo wa
Benki ya dunia wenye thamani ya dola za kimarekani Milioni 410,malengo ya mradi
huu ni kuboresha miundombinu ya miji 45 ya Tanzania pamoja na kujengea uwezo Taasisi
ili ziweze kujiimarisha katika usimamizi wa uendeshaji miji pamoja na
ukusanyaji wa mapato”,anasema.
Alisema
lengo kuu la mradi huo ni kuboresha usimamizi wa ukuaji wa miji pamoja na kuziwezesha
Halmashauri za miji na majiji kutoa huduma bora kwa wananchi huku akitaja
maeneo makuu ya mradi huo kuwa ni ujenzi wa miundombinu mbalimbali zikiwamo
barabara,
Mradi huo unatekelezwa kwenye majiji matano ambayo ni Arusha,DodomaMwanza,Mbeya na Tanga pamoja na manispaa 18 ikiwamo manispaa ya moshi na miji 22.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe, amesema Kata ya Ng’ambo ni miongoni mwa kata nane zitakazonufaika na utekelezaji wa mradi wa huo wa TACTIC, unaolenga kuboresha miundombinu ya barabara na mifereji ya maji ya mvua katika Manispaa hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utiaji saini wa mkataba huo wa ujenzi wa barabara na mitaro ya maji ya mvua, Nasombe alieleza kuwa kupitia mradi huo, jumla ya kilomita 14 za barabara za lami na kilomita 4 za mifereji ya maji ya mvua zitajengwa, hatua inayotarajiwa kubadilisha sura ya mji wa Moshi na kuongeza hadhi ya maeneo ya pembezoni.
Aidha, alibainisha kuwa Kata ya Ng’ambo pia ni eneo linalojengwa Hospitali kubwa ya wilaya yenye ghorofa, ambayo ni ya kisasa na ya kwanza ya aina hiyo katika mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema kuwa mradi huo ni hatua muhimu ya kuondoa kero ya miundombinu duni kwa wakazi wa Manispaa ya Moshi, hususani walioko pembezoni mwa mji.
Babu aliwataka wakandarasi waliokabidhiwa kazi hiyo kuhakikisha wanatekeleza mradi huo kwa viwango vya juu kama walivyoaminiwa na serikali, ili kufikia matarajio ya wananchi wanaosubiri kwa hamu kuona barabara bora na mifereji thabiti ya kupitisha maji ya mvua.
Hata hivyo, Mkuu huyo
wa mkoa alikemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi wanaojihusisha na wizi wa
vifaa vya ujenzi kutoka kwa wakandarasi, hali inayochelewesha utekelezaji wa
miradi.
"Zipo tabia mbaya sana, wakandarasi wamekuwa wakilalamika kuwa vifaa kama mafuta na nondo vinapotea, hii siyo sawa, ni vyema tukalinda na kuthamini uwekezaji huu wa serikali kwa manufaa ya wote," alisisitiza Babu.
Mradi wa TACTIC
unatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya miundombinu ndani ya
Manispaa ya Moshi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali ya awamu ya sita
kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi mikubwa ya maendeleo.




0 Comments