MOSHI-KILIMANJARO
JUMAPILI
ya Septemba 28 mwaka huu wa 2025 Kwaya maarufu ya Mamajuzi ya Kanisa la
Anglikana Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro itasherehekea jubilee ya kutimiza miaka
50 tangu kuazjshwa kwake mwaka 1975.
Hili ni tukio linavuta hisia za watu wengi
katika mji wa Moshi na ukanda mzima wa Afrika Mashariki hasa ikizingatiwa kwa
baadhi ya waimbaji maarufu wa nyimbo za Injili wamepitia hapa.
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Rose Muhando
ni matunda ya kwaya ya Mamajusi kwani wimbo wake wa kwanza wa Homa ya Dunia
ndiyo ulikuwa wimbo wa kwanza kurekodiwa katika studio ya Kasambala iliyokuwa
chini ya Nabii Mkuu Dkt. Geor Davie.
Mwenyekiti wa Kwaya ya Mamajusi,Tito Sambai
anasema katika mahojiano na waandishi wa habari mjini moshi kwa,wimbo huo wa
Homa ya Dunia ndiyo wimbo uliitangaza Mamajusi dunaini.
Anasema yote hayo ni kutokana na Baraka za
Nabii mkuu Geor Davie ambaye wakati huo alikuwa akiwahudumia na kikombe cha
plastiki nyumbani kwake huku akiwa amemshika mkononi mtoto wa Rose Muhando
wakati akirekodi wimbo huo.
Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa zipo faida
nyingi sana katika kumtumikia mungu akisema kuimba kunaokoa,kuimba kunaponya na
pia kuimba kunahuisha.
Anasema kwa miaka hiyo 50 ya Jubilee ya Kwaya Mamajusi kumetoa fursa nyingi katika kuhubiri Injili kwenye nchi mbali mbali za Afrika zikiwamo,Malawi,Unganda,Kenya,Rwanda na Mji wa Butembo uliopo mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki kaskazini katika Jamhuri ya Kimekrasia ya Congo.
Anasema hadi sasa Kwaya ya Mamajuzi inazo
Audio 18 na Video sita huku Video ya saba ikiwa jikoni jambo analosema ni
mafaqnikio makubwa sana katika kueneza Injili kupitia uimbaji
Frederick Mneney ni moja wa waliokuwa wapiga
gitaa wa Kwaya ya Mamajusi ambaye kwa sasa amestaafu,anasema kazi kubwa
imefanyika katika kuenza Injili kupita uimbaji .
Anasema uwepo wa kwaya ya Mamajusi kulifungua
fursa za kuamzishwa kwa kwaya nyingi kwaya anayodai ilikuwa ya pili kuanzishwa
baada ya ile ya Utatu mtakatifu iliyoanzishwa mwaka 1972.
Anasema wazo la kuanzishwa kwaya hiyo
kulitokana na mwaliko wa kwaya ya Upendop St.James ya Arusha ambayo ilitoa
burudani ya kutoka ikkiwa na vyombo vizuri vilivyowasukuma na wao kuanzisha
kwaya hiyo.
Donald Nelson Mtowe ni mwalimu mwanzilishi wa
kwaya ya Mamajusi na mtunzi wa nyimbo za Mungu kaumba dunia,Bwana Uliwaita na Meshack.
Anasama anafurahia uwepo wa kwaya hiyo
aliyoifundisha na pia nafurahia Maajusi kushereheka Jubilee ya miaka 50 tangu
kuanzishwa kwake aksema kwake yeye ni fahari kubwa sana.
Anatoa wito kwa vijana kumjua mungu kwa kwenda kanisani na kuwaasa kuachana na mambo ya dunia ikiwamo matumizi ya dawa za kulevya,uasherati na ulevi wa kupindukia.




0 Comments