MOSHI -KILIMANJARO
MRAJIS wa vyama vya Ushirika nchini,Dkt.Benson Ndiege ametoa wito kwa wananchi wa mikoa ya kanda ya kaskazini hususani mkoa wa Kilimanjaro kutumia Tamasha la kahawa(Kahawa Festival)kurudisha hadhi ya zao la kahawa katika mkoa wa Kilimanjaro.
Wito huo ameutoa katika ufunguzi wa Tamasha la sita la kampeni ya kuhamasisha unywaji wa kahawa nchini linaloendelea kwa siku tatu mfululizo mjini moshi kwenye kiwanda cha kukoboa kahawa cha Tanganyika Coffee Curing Co.
Alisema huwezi ukaelezea mafanikio ya ushirika nchini ukaacha kuvitaja yama kongwe vya ushirika nchini kama (KNCU) ambacho ni chama kikuu cha ushirika mkoa wa kilimanjaro,(NYANZA)chama kikuu cha ushirika mkoa wa Mwanza na SHIRECU ambacho ni chama kikuu cha ushrika mkoa wa Shinyanga.
"Hatuwezi kwenda pamoja kama kaulimbiu yenu inavyosema wakati wadau wengine hatupo nao pamoja,hapa,siwaoni KDCU,Mbinga na wengineo hawa ni wadau muhimu sana kwenye tukio hili",allisema Mrajis.
Mrajis huyo aliwataka pia wakulima kupitia vyama vyao vya msingi kutumia fursa ya miche bora ya mibuni inayotolewa bure na Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB)ambayo haishambuliwi na kutu ya churebuni kupanda kwa lengo la kupata kahawa nyingi na bora.
Alisema miche hiyo bora ya kahawa inamazvuno mengi na kwamba matokeo yake hayawezi kuonekana ndani ya muda mfupi bali yanaonekana baada ya miaka mitatu hadi mitano.
“Bodi ya kahawa haiwezi ikasambaza miche ya kahawa peke yake lazima ishirikiane na vyama vya ushirika wito wangu ni kwenu nyie wakulima kupitia vyama vyenu vya ushirika,pandeni miche bora ya kahawa inayosambazwa na bodi ya kahawa”,alisema.
Akatoa wito kwa maofisa ugani kwenda kwa wakulima kutoa elimu juu ya namna ya kuzalisha kahawa kwa tija huku akitaka kampeni ya unywaji wa kahawa nchini iwe endelevu na kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Bodi ya kahawa kuanzisha kampeni ya unywaji wa kahawa.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Kahawa Tanzania(TCB),Profesa Aurelia Kamuzola alisema zao la kahawa limekuwa na
mchango mkubwa sana kwa uchumi wa wananchi wa Tanzania zao ambalo limewawezesha wananchi wengi kuwa na maisha mazuri.
Profesa Kamuzola alisema kupitia zao la kahawa wananchi wengi wameweza kujenga nyumba bora za makazi,kusomesha watoto wao hii yote ni kutokana na mapato yatokanayo na zao la kahawa.
Alisema jukumu la Bodi ya Kahawa ni kusambaza micho bora kwa wakulima pamoja na kupeleka wataalamu kwa wakulima kutoe elimu ya ugani na kuongeza mnyororo wa thamani kwenye zao la kahawa.
Mkurugenzi wa Bodi ya Khawa Tanzania(TCB),Primus Kimaryo amesema bodi yake inaendelea kutoa elimu kwa wakulima wa zao la kahawa namna ya utunzaji bora wa kahawa kuanzia shambani hadi mnadani .
Alisema kumekuwepo na changamoto kwenye ubora wa kahawa unaotokana na maandalizi duni ya kahawa changamoto inayopelekea kahawa kuwa na muonjo tofauti licha ya kuwa katika daraja moja.
0 Comments