HIVI NDIYO IBRA LINE ANAVYOGUSWA NA CHANGAMOTO ZA WANA MOSHI,ANATUMIA ASLIMIA 80 YA KIPATO CHAKE KUSAIDIA JAMII

 Mgombea ununge wa tikiteti ya Chama cha mapinduzi(CCM),Ibrahimu Mohamed Shayo(kushoto)akiteta jambo na mgombea udiwani kata ya Mji Mpya (CC)Abuu Mohamed Shayo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika  eneo la Mchomba kata ya mji mpya,wawili hawa ni mtu na kaka yake. 

                 MJI MPYA-MOSHI. 

Mgombea ubunge wa Jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ibrahim Shayo, amefichua siri ya kutaka kuwa mwakirishi wa wananchi wa  jimbo la Moshi mjini katika bunge lijalo endapo wananchi watampa ridhaa ya kwaongoza. 

Akizungumza katika mkutano wa kampeni eneo la Mchomba kata ya Mji mpya ,mgombea huyo na mmoja wa wafanyabiashara maarufu katika sekta ya usafrishaji na sekta ya mafuta,Shayo maarufu kwa jina la ‘Ibra Line’,alisema amekwua akitua aslimia 80 ya kupato chake kusaidia jamii ya wana moshi. 

 Aliwaambia wananchi waliokusanyika kaitka mkutano huo kuwa anahitaji kura zao ili akawe mtumishi wao na mtu atakayekwua sauti kwao ya kuwasemea changamoto zao . 

 Shayo  alisema kuwa uwezo wake wa kusaidia haukutokana na madaraka, bali ni moyo wake wa kujitoa kwa jamii na kuongeza kuwa haendi bungeni kutaufta pesa bali anakwenda bungeni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi . 

"Asilimia 80 ya mapato yangu nayatumia kusaidia jamii, kama nimeweza kufanya hivi kabla sijawa mbunge, nichagueni niwe mwakilishi wenu bungeni, nami nitafanya mara mbili ya kile nilichokuwa nikitoa hapo awali," alisema Shayo. 

Aliahidi kushughulikia changamoto ya miundombinu ya barabara katika maeneo ya pembezoni mwa mji wa moshi , akisema kuna maeneo mengi ambayo yamesahaulika na yanahitaji uboreshaji wa haraka ili kuwezesha huduma bora kwa wananchi. 


"Mpeni kura za ndiyo Abuu Shayo",naamu,ndivyo unavyoweza kusama pale mwneyekiti wa ccm moshi mjini,Faraj Swai(kulia)alipomnyanyua mgombea wa kiti cha udiwani kaya ya Mjii Mpya Abuu Shayo.

Aliwaomba wananchi wa kata ya Mji Mpya na moshi kwa ujumla kumpa kura za kishindo mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pia alimwombea kura mgombea udiwani wa kata hiyo ya Mji Mpya Abuu Mohamed Shayo ambaye ni kaka yake wa kuzalwia, akimtaja kama kiongozi mwenye maono makubwa aliyefanikisha maendeleo makubwa katika kata hiyo. 

"Rais Samia ametuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya inayojengwa kata ya Ng’ambo, pia ametuwezesha kukarabati shule kongwe, ni wakati wetu sasa kumrudishia heshima kwa kumpa kura nyingi," alisema

 

wanachama wa chama cha mapinduzi(CCM)kata ya Mji Mpya wakifuatilia mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge wa tiketi ya chama hicho,Ibrahim Shayo

 

Post a Comment

0 Comments