TRA K’NJARO YAZINDUA DAWATI MAALUMU LA UWEZESHAJI BIASHARA

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Hassn Babu(wa pili kutoka kushoto)akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Dawati Maalumu la uwezeshaji biashara mkoa wa kilimanjaro,uzinduzi huo ulifanyika makao makuu ya TRA Kilimanjaro.  

                                     MOSHI-KILIMANJARO 

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro imezindua dawati maalumu la uwezeshaji biashara likiwa na lengo la kutoa huduma karibu kwa wafanyabiashara na kusikiliza na kutatua changamoto zao. 

Dawati hilo limezinduliwa septemba 23 mwaka huu na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Hassan Babu na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwamo wafanyabiashara. 

Akizundua Dawati hilo,mkuu huyo wa mkoa alisema kuzinduliwa kwa Dawati hilo kutaondoa vikwazo vya kibiashara,kutoa elimu ya kodi na kusaidia sekta binafsi kukuza uchumi wa ndani kupitia mazingira rafiki ya biashara. 

Alisema kupitia dawati hilo wafanyabiashara watapata taarifa sahihi kwa wakati,kuelewa wajibu na haki yao  ya kodi na kupata suluhisho la changamoto wanazokutakana nazo. 

Aliwataka wafanyabiashara wote wa mkoa wa Kilimanjaro kulitumia dawati hilo ipasavyo kwa ushirikiano wa kujenga mazingira yenye uwazi,haki na staha kati ya serikali na sekta binafsi. 

“Niendelee kuwakumbusha wananchi wote kuendelea kujisajili,kuwasilisha ritani za kodi kwa wakati,kutoa matamko sahihi kwenye ritani,kulipa kodi stahiki na kwa wakati na kuhakikisha tunadai risiti kilatunaponunua na wafanyabiashara wote kuhakikisha watoa risiti kila wanapouza”,alisema. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema,serikali ya mkoa itaendelea kushirikiana na TRA na Taasisi nyingine kuhakikisha mkoa wa Kilimanjaro unakuwa kitovu cha biashara na uwekezaji kwa kutoa huduma bora,kupunguza urasimu na kuwezesha wafanyabiashara wote kukua. 

Kwa upande wake Meneja wa  TRA Mkoa wa Kilimanjaro, James Jilala, alisema  Dawati hilo litatoa  huduma za karibu kwa wafanyabiashara ikiwamo elimu ya kodi na haki za mlipakodi. 

Alitaja huduma nyingine kuwa ni ufafanuzi wa sheria  na kanuni za kodi,ushauri wa kodi kwa biashara ndogondogo za kati na kubwa pamoja na kupokea na kushughulikia malalamiko na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika shughuli za kila siku.   

Alisema kuzinduliwa kwa Dawati hilo  ni sehemu ya juhudi za serikali kupitiqa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) katika kuhakikisha mazingira kwamba mazingira ya ufanyaji biashara nchini yanazidi kuimarika. 

 Amesema  kupitia dawati hiloTRA inatarajia kuongeza ushirikiano kati ya wafanyabiahsara na mamlaka,pamoja na kuhakikisha changamoto za wafanyabiashara zinatatuliwa kwa wakati,kwa ufanisi na kwa weledi. 

Meneja huyo wa TRA mkoa wa Kilimanjaro alisema kuwa,ushirikiano mzuri kati ya TRA na walipa kodi umechangia mamlaka hiyo kufikia na kuvuka lengo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 la kukusanya Bilioni 301.64 na kukusanya shilingi Bilioni 330.81 ambayo ni ufanisi sawa na aslimia 110. 

“Tunaamini kwa dhati kuwa maendeleo ya kweli ya taifa letu hayawezi kufikiwa bila sekta binafsi imara na inayowezeshwa ipasavyo,dawati hili linajengwa kama daraja kati ya serikali na wafanyabiashara kwa lengo la kujenga mahusiano yenye tija,kuaminiana na kuleta maendeleo ya pamoja”,alisema. 

Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)mkoa wa Kilimanjaro,james Jilala(kushoto)akimpa zawadi Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Hassan babu muda mfupoi mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua rasmi Dawati maalumu la uwezeshaji biashara kwenye makao makuu ya mamlaka hiyo mjini moshi.

 


Post a Comment

0 Comments