MOSHI-KILIMANJARO
HOSPITAL ya Rufaa ya Kanda ya kaskazini ya KCMC,imezindua
kampeni ya siku 90 kusaka fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi mkubwa wa ujengo
la jengo la matibabu na upasuaji wa Moyo unaotarajiwa kugharimu shilingi
bilioni 12.2.
Uzinduzi huo umefanyika huku shirika la afya
duniani(WHO)likisema magonjwa ya moyo ndiyo yanayosababisha vifo vingi duniani
ambapo zaidi ya watu milioni 20.5 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa ya
moyo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Hassan Babu aliyekuwa mgeni
rasmi katika uzinduzi huo alisema serikali inatambua umhimu wa afya kwa binadamu na
kwamba serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
imeimarisha kwa kiwango kikubwa suala la Afya.
Alisema uwepo wa jengo la matibabu ya moyo katika ukanda huu wa
kaskazini pamoja na wataalamu wa kutosha na vifaa itapunguza gharama za
matibabu ya moyo kwa wananchi.
Mapema Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanlink Health Care
Foundation,Siraj Mtulia.aslimia 30 ya vifo vinavyotokea hapa nchini vinatokana
na magonjwa yasiyoambukiza ikiwamo magonjwa ya moyo.
Alisema kulingana na utafiti uliofanywa mwaka 2007 na Taasisi
ya Open Heart International(OHI) Tanzania ilihitaji kuwa na vituo 40 vyenye
hadhi kama Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) vyenye kutoa huduma ya
matibabu ya upasuaji wa kibingwa na bobezi ya moyo kulingana na idadi ya watu
waliokuwepo wakati huo.
“Kutokana na hayo yaliyozungumzwa hapo juu,Tanlink Health Care
Foundation imeona ina kila sababu ya kuunga mkono jitihada za dhati
zinazotolewa na Hospital ya KCMC katika kumaliza kituo cha huduma za kibingwa
na bobezi za moyo katika kanda ya kaskazini na Tanzania kwa ujumla kwa
kukamilisha jengo hili “,anasema.
Alisema kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia kuokoa maisha ya
maelfu ya watanzania hasa watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo,kupunguza
idadi ya wagonjwa wanaosafiri nje ya nchi kutafuta huduma za moyo.
“Kampeni hii siyo ya Taasisi moja pekee,hii ni safari ya pamoja,tunahitaji kila mmoja kushiriki iwe kwa kuchangia fedha,raslimali,au hata kwa kuwa balozi wa ujumbe huu,kauli yetu ni ‘kila pigo la moyo ni Thamani,kila uhai ni muhimu”,alisema.
Taasisi hiyo ya Tanlink Health Care Foundation ilianzishwa kwa dhumuni la kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watanzania ikiwa na majukumu manne.
Majukumu hayo ni pamoja na kutunza na kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya afya ya msingi na ya kibingwa,kuwezesha ushirikiano kati ya sekta binafsi,serikali na Taasisi za kimataifa kwa ajili ya miradi ya kiafya.
Majukumu mengine ni kuendeleza tafiti za elimu ya afya,sambamba na kampeni za kintga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama vile moyo,kisukari na saratani.
Jukumu la nne la Taasisi hiyo ni kusaidia uanzishwaji na uendelezaji wa huduma za matibabu ambazo zina tija kwa wananchi,hasa wale wa kipato cha chini.
Kwa upande wake Mkurgenzi mtendaji wa Hospital ya Rufaa ya
kanda ya KCMC,Profesa Gileard Masenga amesema mradi huo wa jengo la matibabu na upasuaji wa kibingwa na bobezi ya moyo ni wa kimkakati na wa kitaifa na
ukikamilika utakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 100 kwa wakati mmoja.
Alisema pia mradi huo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia
zaidi ya wagonjwa 14,000 kwa mwaka ,kutoa huduma kamili za moyo(comprehensive cardiac
care)kwa wananchi wa kanda ya kaskazini na nchi kwa ujumla.
Alisema hadi sasa ujenzi wa mradi huo upo kwa aslimia 40
ambako washirika wa kimataifa wa KCMC
wamechangia kiasi cha shilingi Bilioni 9.1 sawa na aslimia 75 na kusema kwa sasa kiasi
cha shilingi Bilioni 3.1 zinahitajika kukamilisha na kuanza kutolewa kwa
huduma.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa,magonjwa ya moyo ni miongoni
mwa magonjwa yasiyoambukiza(NCDs)yanayoongoezeka kwa kasi nchini ambako
wagonjwa wengi hulazimika kusafiri kwenda Dar es salaam kwenye Taasisi ya moyo
ya Jakaya Kikwete(JKCI) jambo linalosababisha msongamano mkubwa na gharama kwa familia.
“Mheshimiwa mgeni rasmi mradi huu utasaidia utambuzi wa awali(Early Detection)wa magonjwa ya moyo,kupunguza msongamano wa wagonjwa JKCI na kuokoa maisha ya maelfu ya watanzania kila mwaka “alisema.
Alipogeza serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia
Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na Hospital yake ikiwamo kulipa
mishahara ya watumishi,kutoa fedha za maendeleo na kugharamia mafunzo ya
wataalamu na kuongeza kuwa ushirikiano huo ni dira na faraja kubwa kwa KCMC.
“Wafadhili na wadau wetu wa nje wana imani na mradi huu kwa sababu serikali inautambua,tunashirikiana na serikali imeahidi kulipa mishahara ya watumishi wote watakaofanyakazi katika mradi huu”,alsiema.
Katika uzinduzi huo,ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro imechangia shilingi Milioni tano huku mkuu wa mkoa mwenyewe akichangia shilingi lakini tano na wadau wengine zikiwamo Taasisi zilizo chini ya KCMC ambazo ni KCRI,GSF.




0 Comments