MWAMBA MORRIS MAKOI
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Moshi Vijijini,Cyril Mushi(Kulia)akimkabidhi Ilani ya Uchanguzi ya chama hicho ya 2025-2030 mgombea ubunge Jimbo la Moshi Vijijini,Morris Makoi(kushoto)wakati wa uzinduzi wa kampeni zilizofanyika kata ya Kindi.
MOSHI-KILIMANJARO
MGOMBEA wa kiti cha Ubunge jimbo la moshi Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM),Morris Makoi amezindua rasmi kampeni zake huku akitaja vipaumbele vinane atakavyoanza navyo kama wananchi watampa ridhaa ya kuwatumikia.
Alizindua kampeni zake katika uwanja wa michezo kwenye kata ya Kindi uzinduzi uliofana kwa kiwango kikubwa huku ukihudhuliwa na idadi kubwa ya makada wa chama hicho waliokuwa miongoni mwa watia nia katika jimbo hilo.
Makoi alitaja vipaumbele vyake ikiwamo sekta ya barabara akieleza kuwa barabara ni daraja la maisha na kwamba bila barabara nzuri,mazao ya wakulima hayatafika sokoni kwa wakati,wagonjwa kushindwa kufikishwa hospital haraka na watoto kushindwa kufika shuleni.
“Kama mbunge wenu nitakahakikisha barabara kuu zinazounganisha vijiji na kata zinajengwa kwa kiwango kinachodumu muda mrefu,tutanunua mitambo kama greda,shindilia n.k kwa ajili ya kutengeneza barabara zetu wenyewe tukishirikiana na tarura”
“Barabara zatu kupitika kirahisi tutashirikiana na Tanroads na Tarura kuhakikisha Moshi Vijijini haibaki nyuma katika barabara zake za ndani”,alisema Morris ambaye muda wote wa hutuba yake alikuwa akishangiliwa na umati mkubwa uliojitokeza kwenye uzinduzi huo.
Kuhusu elimu alisema, “Elimu ndiyo urithi bora tunaowaachia watoto wetu,sitaki kuona mtoto wa Moshi Vijijini anakaa darasa la wanafunzi 150 peke yake,mikakati yangu ni kujenga na kukarabati shule za msingi na sekondari”.
“kuimarisha upatikanaji wa vitabu na vifaa vya maabara,kuhamasisha vijana kusoma masomo ya sayansi na ufundi ili tuzalishe wahandisi,madaktari na wataalamu”
Ummy Nderiananga(kushoto),Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu sera,bunge na uratibu akimuombea kura mgobmea ubunge jimbo la moshi vijijini(ccm),Morris Makoi wakati wa uzinduzi wa kampeni zilizofanyika kata ya Kindi.Akizungumzia suala la Afya Morris Makoi amesema afya ndiyo msingi wa maendeleo na kueleza kuwa mkakati wake kwa kushirikiana na serikali ni kuongeza vituo vya afya vyenye dawa,vifaa na wataalam wa kutosha .
Mkakati mwingine ni kuhakikisha zahanati na vituo vya afya vinaboreshwa kwa vitanda,dawa na magari ya wagonjwa huku akigusia huduma ya mama na mtoto kupewa kipaumbele ili kuwawezesha kina mama wajawazito hawatembei umbali mrefu kutafuta huduma.
Alligusia pia huduma ya maji ambako aliahidi miradi ya maji vijijini inafika kila kata na kutumia vyanzo vya maji vya mlima Kilimanjaro kwa faida ya wananchi kwa kutumia teknolojia rahisi ya visima mabwawa pale panapowezekana.
Kuhusu nishati ya umeme,Makoi alisema umeme ni msingi wa viwanda,biashara na hata elimu na kwamba vijana hawawezi kuanzisha miradi ya kisasa bila umeme na wanafunzi hawawezi kujisomea usiku bila mwanga.
Kwenye hilo Makoi alimeahidi kuwa kwa kushirikiana na serikali watahakikisha vijiji na vitongoji vyote vinapewa umeme kupitia REA,kutumia nishati ya umeme jadidifu kwenye miradi hususani sola ili kupunguza gharama za umeme.
'Mwamba'Morris Makoi na mkewe wakiwa wameshika ilani ya uchaguzi ya 2025-2030 wakati wa uzinduzi wa kampeni za kusaka ubunge katika jimbo la Moshi Vijijini.Kuhusu mikopo ya aslimia kumi inayotolewa na Halmashauri,Makoi aliahidi mikopo hiyo inatolewa kwa uwazi bila upendeleo,kuwasaidia wananchi kuanzisha biashara ndogo ndogo na miradi ya kilimo na ufugaji.
Ajira kwa vijana ni moja ya vipaumbele vyake alivyoviainisha kwa wananchi na kwamba mikakati yake ni kuwawezesha vijana kupata mafunzo ya stadi za kazi kupitia VETA na vyuo vya ufundi.
Kuanzisha miradi ya kilimo cha kisasa,ufugaji wa kisasa na ujasiriamali vijijini pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vidogo vitakavyotumia malighafi za ndani ya moshi kama kahawa,ndizi,maziwa na mifugo.
Akizungumzia suala la utawala Bora alisema atahakikisha kila mradi unakuwa wazi na wananchi wanahusishwa huku ripoti za mapato na matumizi zinawasilishwa hadharani kwa wananchi huku akitaka viongozi wa vijiji na kata wawanawajibika kwa wananchi .
“Ndugu zangu nataka moshi Vijijini mpya yenye barabara zinazopitika muda wote,shule znazotoa elimu bora,hospital zenye huduma bora,maji safi na salama,umeme vijijini,vijana wenye ajira na wananchi wanaoshirikishwa kwenye maamuzi ya maendeleo yao”.alihitimisha hotuba yake.
Makada na wapenzi wa chama cha mapinzudi wakiwa wamenyanyua bendera za chama hicho na mabango ya picha katika uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la moshi vijijini,Morris Makoi.




0 Comments