KISHINDO UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM K’NJA IBRA LINE AKITAJA VIPAUMBELE 5 ATAKAVYOANZA NAVYO

 

 'MWANBA 'IBRAHIM SHAYO(KUSHOTO) AKICHUKUA FOMU YA UTEUZI KUWANIA KITI CHA UBUNGE JIMBO  LA MOSHI MJINI

 

MOSHI-KILIMANJARO

CHAMA  Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Kilimanjaro,kimefanya uzinduzi wa kishindo wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani utakaofanyika oktoba 29 mwaka huu huku mgombea ubunge jimbo la moshi mjini(ccm)Ibrahim Shayo,akitaja vipaumbele vyake vitano atakavyoanza navyo endapo atachaguliwa kuongoza jimbo hilo.

Uzinduzi huo ulifanyika jumatatu septemba 8 mwaka huu katika viwanja vya mpira wa miguu shule ya msingi mandela uliopo kata ya Bomambuzi Manispaa ya moshi na kuhudhuliwa na waziri mkuu mstaafu Frederick Sumaye na mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa,Namelock Sokoine.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni kuashiria ufunguzi rasmi wa pazia la kampeni,Shayo mfanyabiashara maarufu na anayejulikana  kwa jina la Ibra Line,alitaja vipaumbele vitano atakavyoazna navyo pale atakapopewa ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa jimbo la moshi mjini.

Moja ya kipaumbele chake ni kushirikiana na serikali kukamilisha ujenzi wa mradi mkubwa wa stendi kubwa ya kisasa ya mabasi iliyopo eneo la Ngangamfumuni ujenzi ambao umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu.

Ahadi nyingine kwa wananchi wa moshi mjini aliyoitoa ni kuhakikisha mji wa moshi unaendelea kuwa msafi ambako alisema atapigania uwepo wa magari ya kuzoa taka na kuimarisha usafi hasa maeneo ya pembezoni mwa mji.

Ibra line au kaka wa jimbo kama ambayo amekuwa akiitwa na wananchi wa moshi mjini,ameahidi endapo atachakuliwa katika uchaguzi huo mkuu hapo oktoba 29 ni kupigania mji wa moshi kuwa jiji ndoto ambayo imekuwa kwenye vichwa vya wanamoshi kwa muda mrefu.

Katika kudhihirisha hilo,alisema atashirikiana na wananchi wa moshi vijijini kupitia kwa mbunge wao ili wakubali sehemu ya ardhi yao kumegwa na kuingizwa moshi mjini ili kukamilisha mchakato huo wa kuifanya moshi kuwa jiji.

Mgombea huyo wa kiti cha ubunge katika jimbo la moshi mjini,alionyesha pia kutoridhishwa na hali ya barabara hasa zilizopo pembezoni mwa mji wa moshi na kuahidi kupambana kuhakikisha zinaboreshwa na kuendana na hadhi ya mji wa moshi.

Baada ya uzinduzi huo wa kampeni,mgombea huyo ameanza rasmi kampeni zake akianzia kata ya Korongoni ambako pia atatumia nafasi hiyo kumnadi mgombea udiwani wa kata ya korongoni kupitia chama cha mapinzuzi(CCM)na kuendelea katika kata nyingine 20 za jimbo la moshi mjini ambako CCM imesimamisha wagombea udiwani kwenye kata zote.  

Post a Comment

0 Comments