RC K’NJARO AZINDUA TAMASHA LA SITA LA KAHAWA NA KUONYA UKATAJI OVYO WA MIBUNI

 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Hassaan Babu,akizungumza kwenye uzinduzi wa Tamasha la Sita la kuhamasisha unywaji wa kahawa 

             MOSHI-KILIMANJARO

MKUU  wa Mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Hassan Babu,amezindua Tamasha la sita la uhamasishaji wa unywaji wa kahawa na kupiga marufuku ukataji ovyo wa mibuni iliyozeeka.

Marufuku hiyo ameitoa mjini moshi wakazi akizundua Tamasha hilo tukio lililofanyika makao makuu ya Bodi ya kahawa Tanzania(TBC)mjini Moshi na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa kahawa wakiwamo wakulima.

Wadau wengine walioshiriki tamasha hili ni pamoja na wanunuzi wa kahawa wa ndani nan je ,wakaagaji wa kahawa,wakoboaji wa kahawa kwa maana wenye viwanda vya kukoboa kahawa na wengineo.

Amesema mkoa wa Kilimanjaro unabebwa na zao la kahawa ukiachilia mbali mazao mengine kama ndizi na mahindi hivyo akawataka wananchi wa mkoa huo kulienzi zao hilo.

Alitoa wito kwa wakulima kung’oa mibuni ya zamani iliyozeeka na kupanda miche bora ya kahawa isiyoshambuliwa na wadudu na si kukata mibuni hiyo na kupanda mazao mengine,

Aliwaasa wakulima kuwatumia wataalamu wa kilimo wakiwamo maofisa ugani watakaowapa elimu juu ya kupanda miche bora na kuwaasa vijana kujikita kwenye kilimo cha kahawa badala ya kukaa vijiweni.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kahawa ya Kilimanjaro inao muonjo mzuri na imekuwa ikipendwa na watu wengi dunia hivyo aksisitiza umhimu wa kuitunza kwani kwa sasa bei ya kahawa ipo juu tofauti na miaka ya hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Tamasha hilo,Denis Mahulu anasema lengo la kuandaa tamasha hilo ni katika jitihada za kuongeza soko la ndani la unywaji wa kahawa ambao kwa sasa upo aslimia saba tu huku aslimia 93 ya kahawa yote inayozalishwa Tanzania ikiuzwa nje ya nchi.

Takwimu zinaonyesha  kuwa ,unywaji wa kahawa duniani unatarajia kuongezeka msimu ujao hadi kufikia magunia milioni 179 huku Ulaya,Marekani na Brazil zikiongoza kwa aslimia 2.25 ya unywaji.

Wakati hali ya unywaji wa kahawa duniani ikitarajia kuongezeka.,Tanzania bado inapambana kuona soko la ndani  linaongezeka hadi kufikia aslimia 15 miaka kumi ijao.

Mkurugenzi wa Bodi ya kahawa nchini(TCB)anabainisha kuwa licha ya Tanzania kuwa nchi pekee yenye  viwanda  vya kuongeza thamani hadi kupata kahawa ya mezani,bado unywaji wa kahawa upo chini kwa wastani wa aslimia tano hadi saba.

Mikakati inayowekwa na Bodi hiyo kufikia kiwango hicho ni pamoja na kuwa na soko la uhakika,kupunguza utegemezi wa masoko ya nje,kuongeza ajira kwa wananchi na kuongeza thamani ya zao la kahawa.

 

Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB),Primus Kimaryo akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha la sita la uhamasishaji unywaji wa kahawa 

Post a Comment

0 Comments