MOSHI-KILIMANJARO.
MGOMBEA wa kiti cha Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Ukombozi wa Umma(CHAUMA) katika jimbo la Moshi Mjini, Patrick John Assenga, ametaja vipaumbele vitano atakavyoanza navyo kama wananchi wa jimbo la Moshi Mjini watamchagua kuwa mbunge wao katika uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29 mwaka uu.
Assenga alitangaza vipaumbele hivyo katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya soko la Manyema mjini Moshi, ambao ulihudhuliwa na mgombea wa kiti cha Urais wa Chama hicho, Salumu Mwalimu aliyembatana na baadhi ya wagomvbea ubunge katika majimo ya Moshi mjini, Vijijini na Vunjo.
Alitaja vipaumbele vyake ni pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wa mjini moshi na kuwaondolea kodi ambazo zimekuwa kero kwao, kurejesha heshima ya mji wa moshi iliyotokana na usafi ambao uliuweka mji huo kwenye ramani ya Afrika.
Aliwambia makumi ya wananchi waliojitokeza katika viwanja hivyo kuwa moshi inahitaji mbunge wa kwenda kuwasema Bungeni na si watu wa kwenda kupiga meza bungeni na kusifia serikali na kuongeza kuwa kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali na si kupiga makofi.
“Mimi sitaki kuwa mbunge wa kusifia serikali, kazi ya kusifia tuwachie wananchi, wananchi wa moshi wanazo changamoto nyingi hivyo wanahitaji mtu wa kwenda kuwasemea Bungeni na hii ndiyo kazi nitakayo kwenda kuifanya kama mtanipa ridhaa ya kwenda kuwatumikia,"alisema.
Alisema masoko hayo ya mji wa moshi siyo mazuri huku akidai baadhi ya kina mama wanafanyabiashara katika mazingira ambayo siyo rafiki kwa kuweka bidhaa zao chini huku hali ya vyoo hasa soko la manyema ikiwa si ya kuridhisha licha ya kutozwa pesa kwa ajili ya kujisaidia,
Amesema uchumi wa mji wa moshi na mkoa mzima wa Kilimanjaro umeyumba kutokana na kilimo cha kahawa kupewa kisogo na watu wengi kujikita kwenye kilimo cha parachichi.
Chauma imesimamisha wagombea udiwani katika kata 16 kati ya 21 katika Jimbo la Moshi mjini ambazo ni Msaranga, Ng’ambo, Mawenzi,Miembeni, Korongoni,Majengo,Kiusa, Karanga, Rau, Soweto, Kibpriloni, Bomambuzi, Longuo B, Njoro, Kaloleni na Pasua


0 Comments