Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Moshi Mjini,Faraj Swai(Kushoto)akimnadi mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la moshi mjini(CCM),Ibrahim Shayo(kulia) kwenye uwanja wa mpira wa Reli uliopo kata ya Njoro
MEYA Mstaafu wa Manispaa ya Moshi na mgombea wa kiti cha udiwani Kata ya Njoro(CCM)amewaomba wananchi wa kata ya Njoro kujitokeza kwa wingi siku ya upigaji kura oktoba 29 mwaka huu na kumpa kura nyingi mgombea wa kiti cha Ubunge jimbo la Moshi mjini(CCM)Ibrahim Shayo maarufu kwa jina la Ibra Line.
Kidumo alitoa wito huo september 20 mwaka huu wakati wa mkutano wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani utakaofanyika nchini kote oktoba 29 mwaka huu.
Alisema Ibrahim Shayo amekuwa karibu na wananchi wa moshi kwa muda mrefu na
kuwasaidia katika shida na raha na kuongeza kuwa amekuwa mtu wa kujitoa kila
mara akiwa hana madaraka yoyote.
Mkutano huo ulifanyika kwenye uwanja wa Reli nakuhudhuliwa na Ibrahim Shayo ambaye anaendelea na mikutano ya kampeni kwenye kata zote 21 za Jimbo la Moshi Mjini,pia ulihudhuliwa na viongozi wa Chama cha mapinduzi moshi mjini wakipngozwa na mwenyekti,Faraj Kibaya Swai.
Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi(CCM),moshi mjini Faraj Swai(Kushoto)akimnadi mgombea wa kiti cha udiwani kata ya NJoro(CCM),Zuberi Abdallah Kidumo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Reli kata ya Njoro.
IBRAHIM SHAYO ANENA
Akizungumza katika mkutano huo,mgombea huyo wa Kiti cha Ubunge jimbo la moshi mjini kwa
tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM,Ibrahim Shayo ametaka wananchi wakata ya
Njoro kukipa kura nyingi chama cha mapinduzi nakukipa ridhaa ya kuwatumikia kwa
kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.
Alisema serikali ya awamu ya sita chini ya jemedali Rais
Dkt.Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa katika kipindi cha miaka minne
ikiwamo utekelezaji wa miradi mikubwa ya
kimkakati.
“Naomba niwaambia ndugu zangu tunaye rais mwenye upendo wa
dhati,mwenye hofu ya mungu,mnyenyekevu na mpenda watu,naombeni tukampe kura
nyingi za ndiyo oktoba 29”,alisema.
Pia alisema endapo wananchi wa jimbo la Moshi mjini watampa kura
na kumpa ridhaa ya kuwaongoza atahakikisha anashirikiana na madiwani
watakaochaguliwa kushughulikia kero zinazowakabili wananchi wa moshi mjini.
Alisema wananchi wa jimbo la moshi mjini wakiwamo wananjoro
wanazochangamoto nyingi ikiwamo changamoto ya miunombinu ya barabara,afya,elimu
na huduma ya uzoaji wa taka.
Alisema atahakikisha ndani ya siku 60 za ubunge wake anapambana kuzishughulikia changamoto hizo kwa kushirikiana na serikali kuu pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya moshi.
Hawa ni makamanda wa chama cha mapinduzi(CCM),Ibrahimu Shayo(kushoto) na Zuberi Kidumo(Kulia)hapa wapo kwenye mkutano wa kampen kata ya Njoro wakinadi sera za CCM na lengo lao ni moja tu nalo ni kuhakikisha chama cha mapinduzi kinapata ushindi wa kishindo kwa nafai ya Urais,Ubunge na Udiwani na kuwatumikia watanzania kwa miaka mitano mingine
Alizungumzia pia suala la miundombinu ya barabara na kuahidi
kushughulikia baadhi ya maeneo yenye changamoto hiyo na kuongeza kuwa atakwenda
bungeni kujenga hoja ili serikali iongeze fedha kwenye miundombinu ya barabara
katika mji wa moshi.
“Mheshimiwa Rais wetu amefanya mambo mengi mazuri katika mji
wetu wa Moshi,ametuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospital yetu ya wilaya
inayojengwa kata ya Ng’ambo,ametuletea fedha zikakarabati shule zetu kongwe za
sekondari,leo ukienda Mawenzi Sekondari madhari ya shule hiyo ni kama makazi ya
mtu binafsi”,alisema.
Aliwataka wanamoshi kumpa kura nyingi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili nae apate nguvu ya kwenda kumlilia shida za wanamoshi pale atakapochaguliwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo wa Oktoba 29 mwaka huu.
Kina mama na kina baba wkaifuatilia mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu kwenye kata ya Njoro Moshi mjini ambako mgombea wa kiti cha Ubun(CCM)brahim Shayo akiwahutubia
Kaka wa jimbo Ibrahim Shayo akizungumza na wananchi wa Kata ya Njoro kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini okotoba 29 mwaka huu





0 Comments