HIVI NDIVYO MOTO ULIVYOITEKETEZA NYUMBA YA ROOM 12 KIUSA MOSHI ,ZIMAMOTO WANUSURU NYUMBA KADHAA KUSHIKA MOTO

                                      MOSHI -KILIMANJARO


Jumamosi ya oktoba 11 mwaka huu moto mkubwa ambaochanzo chake hadi sasa bado hakijajulikana uliiteketeza kabisa nyumba yenye vyumba 12 katika mtaa wa Kusa Line kata ya Kiusa manispaa ya Moshi na kuziacha familia zilizokuwa zikiishi  humo kukosa mahli pa kuishi.

Hata hivyo juhudi kubwa zilizofanywa na kikosi cha Zimamoto na uokoaji kwa kushirikiana na gari la zimamoto kutoka kiwanda cha Sukari cha TPC ziliepusha kutokea kwa maafa makubwa ambayo yangesabishwa na moto kushika nyumba nyingi za jirani ikiwamo Baa maarufu ya Mkulima ambayo imeshikana kwa karibu na nyumba iliyoteketezwa na moto.

Jeshi la Zimamoto kupitia kwa kaimu Mkuu wa kikosi hicho,Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto,Jeremiah Mkomangi likatoa rai kwa wananchi kutoa taarifa mapema za matukio ya moto kwa kutumia namba ya dharura 114 badala ya namba ambayo walitumia kupiga ya 112 ili kuweza kuepusha madhara zaidi kutoea

 

Kadama24 blog ilikuwa live katika tukio hilo na hapa inakuletea tukio hilo  katika picha


mwonekano wa Baa maarufu ya Mkulima ambayo imepakana kabisa na nyumba iliyoteketea kwa moto,juhudi kubwa zilizofanywa na wananchi kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Baa hiyo ziliinusuru isishike moto.


magari ya vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka manispaa ya Moshi na kutoka kiwanda cha sukari cha TPC yakiendelea na zoezi la kuzima moto kwenye nyumba moja mtaa wa Kiusa line Manispaa ya Moshi Jumamosi Oktoba 11 mwaka huu,hata hivyo nyumba hiyo ileteketea kabisa kwa moto 






 

Nyumba inayosimamiwa na watoto wa marehemu Domina Jacob Salema iliyopo mtaa wa Kiusa line Manispaa ya Moshi ikiwa imeteketea kwa moto 






Gari la kikosi cha Zimamoto na uokoaji likiwa katika harakati za kuzima moto ulioteketeza nyumba moja mtaa wa kiusa line moshi mjini

Askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji wakivaa mavazi maalumu tayari kwa  zoezi la  kuzima moto 







Post a Comment

0 Comments