.jpg)
MOSHI-KILIMANJARO
WAANDAAJI wa Tamasha la sita pa kampeni ya kuhamasisha unywaji wa kahawa nchini la Kahawa Festival,wamejivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana tangu kuanzishwa kwa Tamasha hilo mwaka 2020.
Denis Mahulu mwenyekiti wa Tamasha hilo anasema kumekuwepo na ongezeko la washiriki mbali mbali wanaoshiriki tamasha hilo ambalo oktoba 5 mwaka huu ilikuwa kilele cha tamasha la sita na kushuhudiwa mwamko mkubwa wa watanzania wakiwamo wakulima,wakaagaji wa kahawa,wanunuzi wa kahawa na wadau wengine .
Anasema katika Tamasha la mwaka huu kumeshuhudiwa ongezeko la washiriki tamasha ambalo lilienda sanjari na semina kwa wakulima juu ya uelewa wa namna ya kukarabati miche ya kahawa,matokeo chanya ya utafiti wa kahawa pamoja na kuelimishwa juu ya sheria mpya ya jumuiya ya Ulaya katika uaandaaji hadi uuzaji wa kahawa kwenye masoko yaliyopo nchi wanachama wa Jumiuya ya Ulaya.
Jumuiya ya Ulaya imetunga sheria kwa wakulima wa kahawa duniani juu ya uzalishaji wa kahawa unaolenga kutunza mazingira katika uzalishaji wa zao la kahawa na sasa vyama vya msingi vya ushiriki nchini kwa kushirikiana na Bodi ya kahawa nchini(TCB)wanaendesha mafunzo kwa wakulima yanayolenga kukidhi matakwa ya sheria hiyo.
Bodi ya kahawa pia imevumbua teknolojia mpya ya uoshaji wa kahawa teknolojia ambayo inafupisha muda wa kuosha kahawa huu ukiwa ni moja ya mikakati ya Bodi hiyo kuwawezesha wakulima kuwa na kahawa bora na yenye kupata madaraja mazuri.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa nchini,Profesa Aurelia Kamuzola anasema teknolojia ndiyo inaipeleka dunia mbele na huo ni moja ya ubunifu ambao unatoa matokeo mazuri na kuiasa jamii kuheshimu ubuni wa kila mtu.
“Kila mtu anapaswa kuheshimu ubunifu wa kila mtu na moja ya ubunifu huu ni uchumi wa kidijitali na mfumo huu wa kidijitali unaondoa udanganyifu,unaondoa ujanjaujanja na sisi kama Bodi ya kahawa tutaendelea kulinda ubunifu huu “,anasema.
Profesa Kamuzola anasema soko la leo la kahawa duniani linahitaji ubunifu na kuhimiza kila sekta kubuni mbinu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuwashauri wakulima wa zao la kahawa kupanda kahawa pamoja na miti katika mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Akifunga Tamasha hilo,mkuu wa wilaya ya Rombo Raymond Mwangwala aliyemwakirish mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin hassan Babu,alisema sekta ya kahawa ni moja ya sekta muhimu katika uchumi wa mkoa wa Kilimanjaro na kuwataka vijana kuchangamkia fursa ya kilimo cha kahawa .
“Tujivunia vitu vya ndani ili hata soko la nje likiyumba tusitetereke pamoja na kahawa kuwa kinywaji cha pili duniani kinachonywewa na watu wengi nyuma ya maji bado soko la ndani linachangamoto”,anasema.
Bara la Afrika lina takribani nchi 25 zinazolima kahawa, ikiwa ni pamoja na Tanzania. huku bara hilo likitajwa kuwa moja ya wazalishaji wakubwa wa kahawa duniani, hasa kahawa aina ya Arabica na Robusta.
Tanzania ni miongoni mwa nchi wazalishaji wakubwa wa kahawa Afrika na zaidi ya aslimia 90 ya kahawa yote huzalishwa na wakulima wadogo na kahawa na huuzwa kwenye masoko ya kimataifa hasa Ulaya na Marekani.
.jpg)
.jpg)


0 Comments