JUMA RAIBU :SERIKALI YA DKT.SAMIA SULUHU HASSAN IMEIPA KATA YA BOMAMBUZI BILIONI NNE

  

Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM),Mercy Mollel(kulia)akimnadi mgombea wa kiti cha udiwani wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)kata ya Bomambuzi,Juma Raibu Juma. 

 

                                           MOSHI MJINI

MGOMBEA  wa Kiti cha udiwani kata ya Bomambuzi katika Jimbo la Moshi mjini kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi(CCM),Juma Raibu Juma,ameelezea mafanikio ya miaka mitano ya udiwani wake na kueleza namna serikali ya Rais,Dkt.Samia Suluhu Hasan ilivyomwaga pesa nyingi kwa ajli ya maendeleo ya kata yake.

Mgombea huyo wa udiwani ambaye kwa sasa hii ni mara yake ya tatu amesema serikali metoe fedha nyingi katika sekta ya elimu,Afya maji na miundombinu ya barabara.


Akizungumza na wananchi wa kata ya Bomambuzi katika mkutano wa kampeni za uchaguzi uliofanyika mtaa wa Relini,JUma alisema serikali imetoa Zaidi ya shilingi Milioni 800 kwa ajili ya uboreshahji wa huduma za afya ikiwamo kituo cha Afya cha Bomambuzi.


Alisema fedha hizo zimesaidia Uboreshaji wa kituo hicho ikiwamo kununua vifa tiba,vitanda,machine ya X -Ray,chumba cha upasuaji,clinic ya meno,ujenzi wa uzio pamoja na ununuzi wa vitanda vya kisasa kwa ajili ya wodi ya wazazi Zaidi ya vitanda 100 na kuajili watumishi wapya wa kada mbali mbali.


Kwenye sekta ya Elimu,Juma Raibu  alisema kuwa serikali iliipatia kata ya Bomambuzi shilingi milioni 576 kwa ajili ya ubhoreshaji  na ujenzi wa shushule ya sekondari ya Bomambuzi huku pia wakipokea Milioni 386 kwa ajili ya uboreshaji wa shule Mshikamano. 

Kwa mujibu wa Mgombea huyo wa kiti cha Udiwani,serikali pia imetoa fedha kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya matundu ya vyoo kwenye shule tatu za msingi za Azimia,Juhudi na Mandela na ujenzi wa matundu ya vyoo kwa ajili ya walimu wa shule hizo.

Pia serikali imetoa zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya Barabara ya ZARA  na barabara inayoanzia msikiti wa Bomambuzi.

Kwenye mikopo inayotolewa na Halmashauri,kata hiyo imepokea zaidi ya Milioni 300 kwa ajiliya mikopo ya kina Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu.

"Nitaendelea kuhakikisha vikundi vya kina mama vinaendelea kupata mikopo,kufunguliwa akaunti na kupata mafunzo ya elimu bora ya utunzajiwa fedha  zinazotolewa na halmashauri ya Manispaa ya Moshi"

"Nitahakikisha tunashiriki kinagaubaga hali ya ulinzi na usalama inaimarishwa ili wananchi waweze kufanyakazi bila usumbufu na bila bughudha yoyote",alisema.


Ameahidi kusimamia uboreshwaji wa soko la Bomambuzi kuhakikisha linakuwa katika kiwango bora na kuongeza tija kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa kuendelea kuwekeza kwenye soko hilo.

katika hatua nyingine Juma Raibu alisema kuwa Mamlaka ya Majisafi na uondoshaji majitaka Moshi Mjini(MUWSA),imetoa zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya uboreshaji wa mfumo wa majitaka ambao ulikuwa kero kubwa kwa wananchi wa kata hiyo na kata jirani ikiwamo Pasua.

Alisema fedha hizo zimetumika kuweka mabomba yenye upenyo mkubwa tofauti na mabomba ya zamani ambayo yalikuwa na upenyo mdogo na kusababisha majitaka mengi kutiririka kwenye makazi ya watu.
wanachama wa chama cha mapinduzi(CCM)kata ya Bomambuzi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea udiwani kata hiyo,Juma Raibu Juma

Post a Comment

0 Comments