IBRAHIM SHAYO ALIA NA UBOVU WA BARABARA ZA PEMBEZONI MWA MJI WA MOSHI,AAHIDI KUPAMBANA NAZO ZIBORESHWE AKICHAGULIWA KUWA MBUNGE

            
                  

 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Kilimanjaro,Mercy Molle(kulia)akimnadi mgombea wa kiti cha Ubunge jimbo la Moshi Mjini(CCM),Ibrahim Shayo kwenye mkutano wa kampeni za ubunge eneo la M-Pesa Kata ya Bomambuzi 


                                                      MOSHI MJINI 

 

MGOMBEA wa kiti cha  Ubunge katika Jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM),Ibrahim Mohamed Shayo maarufu kwa jina la ‘Ibra Line’ameonyesha kukerwa na hali mbaya ya miundombinu ya barabara hasa zilizoko pembezoni mwa mji wa moshi ambazo zimekuwa kero kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo. 

Kutokana na kero hiyo,Shayo mmoja wa wafanyabiashara maarufu nchini katika sekta ya usafrishaji na sekta ya mafuta akimiliki vituo va mafuta,amewaahidi wananchi wa jimbo la moshi kushughulikia kero hizo mara moja endapo watampa ridhaa ya kuwaongoza katika uchaguzi mkuu utakaofanyiuka oktoba 29 mwezi huu. 

Akizungumza na wananchi na wapenzi wa Chama cha mapinduzi(CCM)Kata ya Mbomambuzi katika mkutano wa kampeni eneo la M-Pesa,Shayo amesema barabara za pembezoni mwa mji wa moshi ni mbaya na hazifai kupitika.


                    Kaka wa Jimbo Ibrahim Shayo,a.k.a Ibra Line


“Ninajua shida zenu wananchi wa Bomambuzi,tumepita kwenye hii barabara ya M-Pesa kwa kweli haifai ni chafu  ni mbaya kiasi kwamba magari madogo hayawezi kufika majumbani,tupeni kura oktoba 29 tukazibadilishe miundombinu ya barabara hizi za pembezoni”,alisema. 

Alisema atakwenda kwenye Baraza la madiwani la manispaa ya msohi kujengo hoja kama ni uhaba wa magreda ya kutengeneza barabara basi yanunuliwe mengine ili barabara hizo zitengenezwe ziweze kupitika muda wote . 

Akizungumzia hali ya kituo cha  afya cha Bomambuzi, Shayo alisema kituo hicho kinakabiliwa na  changamoto nyingi ikiwamo  ukosefu wa uzio, chumba cha kuhifadhia maiti, na upungufu wa madaktari, na kuahidi kushughulikia changamoto hizo endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge katika uchaguzi huo wa rais,wabunge na madiwani. 

Aligusia pia ujenzi wa Hospital ya wilaya ambao bado haujakamilika na kuwaahidi wananchi kuweka msukumo kuhakikisha Hospital hiyo inakamilika na wananchi wanapata huduma na kusisitiza hawezi kuwa mbunge asiyekuwana Hospital ya wilaya.

“Nawaomba kwa moyo wa dhati, Oktoba 29, mjitokeze kwa wingi kupiga kura, namuombea kura za kishindo rais wetu,mwenye upendo Dkt. Samia Suluhu Hassan, nipigieni na mimi Ibrahim Shayo kuwa mbunge wenu, pamoja na Dogo Janja Juma Raibu Juma kwa nafasi ya udiwani,” alihitimisha. 

Kuhusu Stendi mpya ya Mabasi ya mkoani ya Ngangamfumuni alisema ujenzi wa stendi hiyo umekuwa wa kusuasua na kuahidi akichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Moshi mjini atakwenda kupigania ujenzi wa stndi hiyo ukamilike kwani ni moja ya stendi itakayochangia ukuajiwa wa uchumi wa mji wa moshi . 

Aidha, alitaja pia mradi wa uwanja mdogo wa ndege wa Moshi ambako amesema atahakikisha uwanja huo unakamilika haraka kwani ni  miongoni mwa miradi mikubwa yenye tija kiuchumi, akisema kukamilika kwake kutafungua mzunguko mkubwa wa fedha na kuongeza idadi ya watalii wanaokuja kupanda Mlima Kilimanjaro.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Kilimanjaro,Mercy Mollel(kulia)akimnadi mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Bomambuzi(CCM),Juma Raibu a.ka dogo janja kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la M-Pesa kata ya Bomambuzi.

 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Kilimanjaro,Mercy Mollel(kulia)akimnadi mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Pasua(CCM),Barreh Farrah kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la M-Pesa kata ya Bomambuzi,Pasua na Bomambuzi ni kata pacha ambapo awali ilikuwa ni kata moja ya pasua kabla ya kugawanywa



 

Post a Comment

0 Comments