Phabian Modest Mallya meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Moshi akipanda mti kando ya msitu wa hifadhi wa Kahe uliopo wilaya ya Moshi Mkoani Kiliamnjaro.
MOSHI KILIMANJARO
BENKI
ya Stanbic imetoa miti 49,000 ikiwa ni mchango wake katika kuunga mkoo juhudi
zinazofanywa na serikali katika kampeni ya uhifahdi wa mazingira katika msitu
wa Kahe uliopo wilaya ya Moshi Mkonai Kilimanjaro.
Miti
hiyo imetolewa na benki hiyo na kukabidhiwa kwa Kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania wadhamini wakuu wa Kampeni ya Twendezetu Butiama ikiwa ni
kuunga mkono juhudi zilizofanywa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
wakati wa uhai wake.
“Niheshima
kubwa kwa niaba ya Stanbic Bank Tanzania kuwa hapa leo tukihitimnisha rasmi
msimu wa 2025 wa Twendezetu Butiama kwa tukio lenye maana kubwa la kupanda
miti”,anasema Phabian Mallya meneja wa Stanbic Bank tawi la Moshi kwa niaba ya
benki hiyo nchini.
Alisema
miti hiyo iliyokabidhiwa nakupandwa kuzunguka msitu wa hifadhi wa asili wa Kahe
itaendeleza dhamira iliyonayo benki hiyo ya kulinda mazingira,kuimarisha maisha
ya jamii na kuiendeleza Tanzania yenye kijani kibichi kwa vizazi vijavyo.
Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Moshi,Phabian Modest Mallya akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kampeni ya upandaji mti katika msitu wa Hifadhi wa Kahe uliopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro,Benki hiyo ya Stanbic imetoa ufadhiri wa miti 49,000 kuunga mkono juhudi za uhifadhi wa mazingira katika msitu huo.
“Kupitia
ushirikiano wetu na Vodacom Tanzania,tumejifunza jambo moja muhimu ,maendeleo
ya kweli hujengwa kwa umoja,ushirikiano na matendo,tunaahidi kuendelea kuwa
mshirika wenu wa maendeleo katika elimu,afya na utunzaji wa mazingira”,alisema.
Msitu
wa hifadhi wa Kahe, ambao upo katika Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro,
umekuwa ukikabiliana na changamoto kubwa kutokana na shughuli za
kibinadamu, na hii inahatarisha ustawi wa msitu huo,msitu ambao umekuwa
muhimu kwa uhifadhi wa bioanuai, hifadhi ya vyanzo vya maji, na uhifadhi
wa udongo dhidi ya mmomonyoko.
Shughuli za kibinadamu zinazohatarisha msitu wa Kahe:
Upanuzi
wa kilimo, hasa kilimo cha mahindi, na mboga, kimesababisha kuvunja sehemu
kubwa ya msitu kwa ajili ya maeneo ya kilimo huku uingizaji wa mifugo
ukitajwa kuchangia uharibifu wa msitu, hasa kwa kulisha mifugo ndani ya
hifadhi, hali inayoathiri ukuaji wa mimea na usawa wa mazingira.
Kasi ya ukataji miti kwa ajili ya uchomaji wa mkaa na ujenzi wa nyumba za makazi ni moja ya sababu zinazochangia kupoteza maeneo ya msitu, ambapo wananchi wanavuna miti na kuiuza kama kuni au mkaa kwa matumizi ya nyumbani na biashara
Mikakati ya kukabiliana na hali hii:
Elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa mazingira ya msitu wa Kahe ni muhimu ili kuwawezesha wananchi kuelewa umuhimu wa msitu wa Kahe kwa jamii zao, kama vile hifadhi ya vyanzo vya maji na faida za bioanuai. Elimu itakayowajengea wananchi ufahamu wa umuhimu wa kulinda msitu.
Uboreshaji wa sheria na usimamizi
Kwa kutambua umuhimu wa msitu huo katika uhifahdi wa manzigira serikali na vyombo vya usimamizi wa hifadhi wanapaswa kuimarisha sheria za uhifadhi wa mazingira, kuhakikisha kuwa kuna udhibiti wa shughuli zote zinazofanyika katika msitu huo. Hii inajumuisha kuimarisha doria za kulinda misitu dhidi ya uharibifu
Kilimo endelevu
Ni muhimu wananchi wakapewa elimu juu ya kuendeleza kilimo cha kisasa na endelevu kinachohakikisha kuwa ardhi inatumiwa kwa manufaa ya kijamii bila kuharibu mazingira. mfano, kilimo cha shamba la miti (agroforestry) ambacho kinahusisha kilimo na uhifadhi wa miti, unaweza kuwa suluhisho bora.
Uanzishaji wa maeneo ya hifadhi za jamii
Ni jukumu la wakala wa misitu Tanzania(TFS)ambao ndiyo wasimamizi wakuu wa msitu huo kutoa elimu ya uanzishwaji wa maeneo ya hifadhi zinazohusisha jamii ili wananchi waweze kunufaika na uhifadhi wa msitu kwa kutumia rasilimali za msitu kwa njia endelevu, kama vile utalii wa mazingira au uvunaji wa mazao ya misitu kwa njia endelevu.
Utafiti na ufuatiliaji
TFS inawajibu wa kuendeleza tafiti za kisayansi na ufuatiliaji wa kila mara kuhusu hali ya msitu wa Kahe hii itasaidia kutambua mabadiliko yoyote yanayotokea, ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati.
Kuhusisha serikali za mitaa
Serikali
za mitaa na viongozi wa kijamii wanapaswa kuwa sehemu ya juhudi za kulinda
msitu. Kupitia ushirikiano wa karibu, wananchi wanaweza kusaidia kudhibiti
uharibifu wa misitu.
Kwa kifupi, mikakati inayohusisha elimu, sheria, usimamizi mzuri, na ushirikiano wa jamii inaweza kuwa suluhisho muhimu katika kulinda msitu wa Kahe na kuhakikisha kuwa unaendelea kutoa faida kwa vizazi vijavyo.
Washiriki wa kampeni ya Twendezetu Butiama wakipanda miti kando ya msitu wa Hifadhi wa Kahe wilaya ya Moshi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere katika uhifadhi wa mazingira wakati wa uhai wake






0 Comments