KAMPUNI YA MINJINGU YATOA ELIMU YA MATUMIZI BORA YA MBOLEA KWA WAKULIMA WA KAHAWA,NI KATIKA TAMASHA LA KAHAWA FESTIVAL

 

Afisa masoko wa kampuni ya kuzalisha mbolea za minjingu mkoani kilimanjaro,Abel Ngwagu(kulia)akitoa maelezo mafupi ya matumizi bora ya mbolea za minjingu kwa mkuu wa wilaya ya Rombo,Raymond Mwangwala (kushoto)kwenye tamasha la sita la kahawa(kahawa Festival)mjini moshi

                  MOSHI-KILIMANJARO

KAMPUNI  ya kuzalisha mbolea ya Minjingu ya mkoani Arusha imetumia Tamasha la sita la kuhamasisha unywaji wa kahawa nchini (Kahawa Festival)lililofikia kilele chake jumapili octoba 5 mwaka huu mjini moshi kutoa elimu ya matumizi bora  ya mbolea za minjingu kwa wakulima wa zao la kahawa .

Tamasha hilo la sita la kuhamasisha unywaji wa kahawa limefanyika kwa siku tatu mjini moshi katika kiwanda cha kukoboa kahawa cha Tanganyika Coffee Curing na kuzinduliwa na mrajis wa vyama vya ushirika nchini,Dkt.Benson Ndiege.

Akizungumza na vyombo vya habari katika Tamasha hilo,afusa masoko ya kampuni hiyo ya Minjingu mkoani Kilimanjaro,Abel Ngwagu alisema kuwa,mbolea za minjingu ni mbolea za asili.

Alisema mbolea za minjingu zinatokana na  mabaki ya viumbe hai hivyo ni mbolea inayotunza unyevu pamoja na kutunza ardhi tofauti na mbolea zingine  hivyo mazao hayawezi kunyauka.

“Tupo hapa kutoa elimu juu ya matumizi bora na sahihi ya mbolea za minjingu kwa ajili ya wakulima wa kahawa na wakulima wa mazao mengine kwani mbolea zetu ni za asili zikitokana na mabaki ya viumbe hai”,alisema.

Kwa mujibu wa afisa masoko huyo wa kampuni ya mbolea za minjingu ,mbolea hizo pia zipo kwenye mfumo wa mbolea za ruzuki zikiuzwa kwa bei nafuu kuliko mbolea nyingine ambako mfuko wenye ujazo wa kilogramu 50 wa mbolea ya kupandia NAFAKA DAAP PLUS inauzwa sh,56,456.

Alisema mbolea ya kukuzia yaani CAAN PLUS  mfuko wenye ujazo wa kilogram 50 inauzwa sh,53,414 na kutoa wito kwa wakulima wa kahawa na mazao mengine kutumia mbolea za minjingu kwa ajili ya kupandia na kukuzia.

Kwa faida ya wakulima wa zao la kahawa nchini mbolea aina ya COFFEE PLUS NPK 20:10:15 ambayo ni mbolea ya kuongeza uwezo wa mibuni ina viburudisho vya aina tano.


Abel Ngwagu,afisa masoko kampuni ya kuzalisha mbolea za minjingu mkoani Kilimanjaro akiwa kilele cha Tamasha la sita la Kahawa(Kahawa Festival)mjini moshi

Akihitimisha kilele hicho cha Kahawa Festival,Mkuu wa wilaya ya Rombo,Mwalimu Raymond Mwangwala kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Babu, aliwataka wakulima wa zao la kahawa na wananchi kwa ujumla kujivunia vitu vya ndani.

Alisema ni wajibu wa kila mtanzania kuwa balozi wa kuhamasisha unywaji wa kahawa na kuongeza kuwa kama soko la ndani la kahwa litaimarika vijana wengi watapata ajira.

“Tujivunie vitu vyetu vya ndani ili hata bei ya kahawa kwenye soko la dunia likiyumba tusitetereka lakini pamoja na kwamba kahawa ni kinywaji muhimu na ni cha pili duniani ukiondoa maji bado soko la ndani linachngamoto”,alisema.

Aliwataka watanzania kupuuza propaganda zinazoenezwa na watu kwamba kahawa ina madhara mwilini na kueleza kuwa kahawa inazofaida nyingi mwilini ikiwamo kuchangamsha mwili pamoja na kuondoa msongo wa mawazo. 

Afisa masoko kampuni ya kuzalisha mbolea za Minjingu,Abel Ngwagu (wa pili kutoka kushoto)akipokea tuzo na cheti kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Rombo,Raymond Mwangwala(wa tatu kutoka kulia)kama moja wa wadhamini wa Tamasha la Kahawa Festival mjini moshi jumapili oktoba 5,2025,

Post a Comment

0 Comments