BAJAJ NA BODA BODA K’NJARO WAJITENGA NA VURUGU ZA OKTOBA 29,WADAI WALIOFANYA VURUGU NI WAHUNI

 


WAENDESHA Bodaboda na Bajaj mkoani Kilimanjaro wamekutana na kuzungumzia vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu oktoba 29 mwaka huu zilizosababisha uharibifu wa mali pamoja na vifo na kutoa neno.

Katika mkutano wao wa siku moja kwenye ukumbi wa mikutano makao makuu ya polisi usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,wamesema waathirika wakubwa wa uvunjifu wa Amani ni madereva wa Bodaboda na Bajaj na kuiambia dunia kuwa hawahusiki na vurugu hizo ambazo ziliwaathiri kwa kiwango kikubwa.

Bahati Nyakiraria mwenyekiti wa Bodaboda na Bajaj mkoa wa Kilimanjaro amesema tukio hilo liliwaathiri kiuchumina kiafya na kwamba waliofanya vurugu hizo kwa kutumia Bajaj na Bodaboda si wao bali ni wahuni waliotumia vyombo hivyo na kujificha kwenye mwamvuli wa Boda na Bajaj.

Alitoa rai kwa wanachama hao kujiepusha na vurugu na kutokujiingiza kwenye uvunjifu waamani kwani wahanga wakubwa wa uvunjifu wa amani ni wao na kutoa wito wa kuwafichua wale wote wanaobainika kupanga na kuchochea vurugu.

“Uvunjifu wa Amani ukitokea wa kwanza kuathirika ni sisi kwa sababu tunabeba abiria,wengi walioathrika ni abiria kwa sababu wanatumia usafiri wetu,wengine waliathirika kiuchumi kiafya na wengine walipata mshtuko “,alisema.

Bahati amesema si kila anayeendesha boda boda au bajaj anafanya kazi kama yao,baadhi wanazitumia kwa malengo yasiyokusudiwa na kuwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa Amani.


Amesema jukumu la kuilinda na kutunza Amani ni jukumu la kila mtu na si kuwaachia vyombo vya ulinzi na usalama wakiwamo polisi,na kuongeza amani ni jukumu la watanzania wote.

Kutokana na matukio hayo ya uvunjifu wa Amani serikali imeanza mchakato wa kuvisajili vyombo hivyo vya moto ili kuwa na udhibiti kwa wale watakaotumia vyombo hivyo kutekeleza uharifu ukiwamo uharifu wa kuoanga .

Akizungumzia hilo Bahati amesema kuwa Bajaj na Bodaboda zitasajiliwa nakuingizwa kwenye mfumo na mamlaka ya uhdibiti wa usafiri ardhini(LATRA) na wale watakaobainika kufanya uharifu mfumo utawakataa.

 Mfumo huo pia utakuwa mwarobaini wa matukio ya uporaji unaofanywa na waharifu ambao wamekuwa wakitumia bodaboda kupora watu katika maeneo mbali mbali nchini



Mwenyekiti wa Chama cha waendesha Bodaboda na Bajaj mkoa wa Kilimanjaro,Bahati Nyakiraria(kulia)akiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Moshi mjini,Hamadi Bendera



 

 


Post a Comment

0 Comments