KIWANDA cha sukari cha TPC kilichopo mkoani Kilimanjaro,kimeanza mkakati wa kuwekeza kwenye sekta ya viwanda itakayowezesha kupanua wigo na kuongeza thamani pamoja na kuongeza ajira baada ya kuanza ujenzi mkubwa wa kongani ya viwanda ambako kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 130 zitatumka.
Mkakati huo wa TPC utafungua fursa za kiuchumi na inatarajiwa kutoa ajira 1,800 zikiwa ajira za kudumu za na muda mfupi .
Kwa muda mrefu TPC imekuwa ikitumia makapi ya miwa katika uzalishaji wa nishati ya umeme na kuokoa mamilioni ya fedha ambazo zingetumika kwa ajili ya kulipia Ankara za umeme kwa shirika la umeme Tanzania(Tanesco)kutokana na kuwa na kiwanda kikubwa cha kuzalisha nishati hiyo ya umeme.
Mtendaji mkuu wa kiwanda hicho anayeshughulikia masuala ya utawala , Jaffari Ally amesema leo novemba 18,2025 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa kongani hiyo kitakachojengwa Kata ya Arusha Chini, Wilaya ya Moshi.
AFISA MTENDAJI MKUU WA KIWANDA CHA SUKARI CHA TPC ANAYESHUGHULIKIA UTAWALA,JAFFARI ALLY AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WAHABARI KUHUSIANA NA UJENZI WA KONGANI YA VIWANDAAmesema ujenzi wa kiwanda hicho ukikamilika utazalisha lita milioni 16.3 za Extra Neutral Alcohol maarufu Ethanol (ENA) na uzalishaji wa lita 400,000 za nishati Technical Alcohol inayotumika katika majiko poa kwa ajili ya kupikia majumbani.
Amesema kongani nyingine, itazalisha mbolea aina ya Potasium, ikakadiliwa kufikia metriki tani 8,000 hii itatokana na kuchakatwa kwa molasesi, baada ya kuzalishwa Ethanol.
Kwa mujibu wa Jaffari,kiwanda hicho pia kitazalisha hewa ukaa lita 400,000 ambayo itakuwa mahususi kwa ajili ya matumizi ya viwandani pamoja na uzalishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme megawati sita zitakazouzwa kwa Tanesco.
Amesma miradi hiyo
inatarajia kukamilika mwezi Desemba mwaka 2026 nakuongeza kuwa miradi hiyo
inakwenda pamoja na uwezo wa TPC ukusanyaji na ulipaji wa kodi pamoja na uboreshaji wa mazingira mazingira lengo ni kusaidiana na serikali katika juhudi zake za
kuwa na nishati salama na safi.
.jpg)

.jpg)
0 Comments