MABAKI ya mwili wa Mtanzania Joshua Mollel, aliyeuawa na kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza miaka miwili iliyopita, yamewasili loe nchini na kupokelewa na ndugu jamaa na marafiki katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa KIlimanjaro (KIA) ukitokea Tel Aviv, Israel.
Kuwasili kwa mabaki hayo ya mwili wa Joshua
inafuatia makubaliano ya kumaliza vita katika ukanda wa Gaza na kuruhusu makabidhiano ya mateka na miili ya waliouawa
kwa pande zote kati ya nchi ya Israel na
Kundi la Hamas kutoka Palestina.
Tayari Israel imepokea miili ya mateka 19
Waisraeli waliorejeshwa na Hamas, pamoja na miili ya mateka watatu raia wa
kigeni,raia mmoja wa Thailand, mmoja wa Nepal na Mtanzania mmoja.
Kwa upande mwingine Israel imekabidhi jumla ya miili 285 ya Wapalestina
ikiwa ni sehemu ya makubaliano hayo yaliyopelekea kutamatika kwa vita hivyo ambavyo vimagharimu maisha ya watu na mali zao huku maelfu wakiyakimbia makazi yao.
Ibada maalumu ya kuaga mabaki ya mwili wa Joshua ilifanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Israel
siku ya jana Jumanne, Novemba 18 kabla ya safari ya kurejeshwa nchini .
Mabaki ya mwili huo
yamepokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa na Balozi Silima Haji Kombo.






0 Comments