KIWANDA cha sukari cha TPC kilichopo mkoani Kilimanjaro ambacho ni moja ya viwanda vya sukari hapa nchini kinachofanya vizuri ,kinajivunia na kusherehekea hatua kubwa ya mafanikio ya miaka 25 tangu kubinafsishwa kwake a serikali .
Hatua hiyo inaashiria safari ya ajabu ya mabadiliko yaliyoofanywa na mwekezaji huyo na kuwa moja ya makampuni inayoongoza katika sekta ya kilimo Afrika Mashariki huku serikali ikijivunia uwekezaji huo ambako inamiliki hisa za aslimia 25 huku mwekezaji akimiliki aslimia 75.
Hafla ya maadhimisho hayo ilifanyika Moshi na kuwakutanisha
viongozi wa serikali , washirika wa kimataifa, wadau wa sekta hiyo, na
wanachama wa jumuiya ya TPC.
Miongoni mwa wageni mashuhuri alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu aliewakirishwa na katibu Tawala (RAS), Msajili wa Hazina , Nehemiah Mchechu, wajumbe wa bodi ya TPC, na wawakilishi kutoka kampuni ya Miwa Sugar Ltd.
Akizungumza kaitka hafla hiyo iliyoenda sanjari na uwekaji jiwe na msingi la ujennzi wa kongani ya viwanda Mwenyekiti wa Kampuni a Miwa Sugar ,Arnaud Lagesse,alitoa shukrani za dhati kwa wafanyakazi, washirika, na Serikali ya Tanzania kwa jukumu lao katika kuunda hadithi ya mafanikio ya TPC.
Lagesse alielezea safari ya miaka 25 ya TPC kama iliyojengwa katika ushirikiano imara, hasa na Serikali ya Tanzania, Quartier Français, na sasa Tereos akieleza ushirikiano huo, unaochanganya uzoefu wa ndani na utaalamu wa kimataifa, umeiwezesha TPC kufikia nguvu ya kiufundi, uongozi wa kimaadili, na athari kubwa kwa jamii.
"Kwa robo karne, ushirikiano huu umeunda mageuko ya TPC,kwa pamoja, tumejenga biashara inayoonyesha ustahimilivu, kusudi la pamoja, na kujitolea kwa muda mrefu," alisema.
Pia aliwapongeza waanzilishi na wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu waliosaidia kubadilisha TPC kutoka kwa biashara ndogo ya sukari hadi kuwa kiongozi wa kikanda anayejulikana kwa tija, uendelevu, na uaminifu.
Kama sehemu ya awamu yake inayofuata ya ukuaji, TPC
imezindua mradi mpya wa kiwanda cha kutengeneza pombe, hatua muhimu ambayo Bw.
Lagesse alisema inawakilisha upya, uvumbuzi, na kujiamini katika mustakabali wa
viwanda wa Tanzania.
Katika Hafla hiyo ,mwenyekiti huyo alitangaza kuingia kwa mshirika mpya, Kundi la Isautier, ambalo utaalamu wake katika utengenezaji pombe na kuongeza thamani unatarajiwa kuimarisha uvumbuzi wa bidhaa za TPC na kufungua fursa mpya za ushirikiano.
"Tunachagua washirika wanaoshiriki maadili yetu na
maono ya muda mrefu,hili ndilo linaloifanya kampuni hii kusonga mbele,"
alisema.
Wakati akisherehekea uzalishaji wa sukari uliorekodiwa wa kampuni hiyo mwaka 2025, Lagesse alisisitiza kwamba mchango wa kweli wa TPC unazidi miundombinu na matokeo na kwamba ni jukumu la kampuni katika kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Moshi.
TPC imewekeza katika shule, huduma za afya, miradi ya
nyumba, na programu za maendeleo ya wakulima wadogo, na kuboresha maisha ya
maelfu wanaotegemea kampuni moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
"Tunaona ni fursa kuchangia katika hadithi ya ukuaji wa
Tanzania. Jukumu letu ni kusaidia kuunda fursa kwa kizazi kijacho,"
aliongeza.
Alisema kuimarisha
ushindani wa TPC, kupanua minyororo mipya ya thamani, na kuunda thamani ya muda
mrefu kwa washirika na wafanyakazi wa Tanzania ndio malengo makuu ya kampuni.
Alibainisha kuwa miongo ijayo italeta changamoto mpya, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, matarajio ya watumiaji yanayobadilika, na mabadiliko ya haraka ya kiteknolojia. Hata hivyo, alionyesha imani katika ustahimilivu wa timu na washirika wa TPC.
"Kwa watu wake, ushirikiano, na ustahimilivu
uliothibitishwa, TPC itaendelea kuongoza kwa kusudi katika uzalishaji,
uendelevu, utawala, na athari za jamii," alisema.







0 Comments