ABIRIA 49 wa Bus la kampuni ya Makupa lenye nmaba za usajili T 958 DRK waliokuwa wakisafiri kutokea Jijini Arusha kwenda Jijini Dar es salaam,wamekwama njiani eneo la njia panda katika mjini mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro tangu jana jioni hadi mchana wa leo .
Mmoja wa abiria aliyezungumza kwa njia ya simu na kadama24blog Ally Bilali amasema baada gari hilo kuharibika majira saa kumi jioni walipiga simu kwa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro kuomba msaada .
Bilal anasema hata baada ya kusubiria kwa saa sita lakini hakupata msaada owowte na hakuna hatua zilizochukuliwa na kuamua kwenda kuomba msaada kituo cha polisi kilichopo kilometa chache kutoka Njiapanda na kuunganishwa na mkaguzi wa polisi aliyetajwa kwa jina moja la Mayunga .
"Tukaambiwa atakuja mkaguzi wa polisi kuja kukagua hiyo gari lakini hakufika abiria kiujumla tunateseka unatoa taarifa mwishowe hakuna msaada tumelala kwenye gari wengine wamelala hotelini ,kweli siyo sawa mmiliki pamoja na dereva wake na konda wa gari hawatoi ushirikiano walitukimbia,"amesema.
"Mimi nilipaswa kuwa kwenye session mahakamani Dar es salaam leo hii lakini leo nipo hapa kwa sababu ya kukwamishwa kwa makusudi maana tangu jana wangeturudishia nauli au kututafutia gari jingine kama ilivyo sheria za usafirishaji,"amesema Bilal
“Leo asubuhi inspector Mayunga anatuambia mmiliki hapatikani tuandike taarifa zetu na maji yetu tutafute usafiri tuondoke atakapo patikana watatuita turudishiwe gharama zetu”
Kwa upande wake Afisa
mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini LATRA mkoa wa Kilimanjaro,Paul
Nyello amesema taarifa juu ya abiria hao wamepokea saa mbili
asubuhi na hatua imechukuliwa ya kutafuta usafiri mbadala,baada ya kuwa dereva
na kondokta kukimbia na mmiliki alipotafutwa kwenye simu na kujulishwa tatizo
la Bus hakutoa ushirikiano baadae simu yake haipatikana tena.
Aidha Nyello amesema hakuna abiria yoyote aliyewasiliana na afisa yoyote wa mamlaka hiyo kuomba ufafanuzi wowote wa kisheria ,na kwa mujibu wa utaratibu anayetakiwa kutoa taarifa ni Afisa Mfawidhi wa mkoa.
Mkuu wa kikosi usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro(RTO) ACP Nassoro Sisiwayah amesema wamefanikiwa kumkamata dereva wa Bus hilo aliyemtaja kwa jina la Ibrahim Athumani na kumweka mahabusu mpaka pale ambapo mmilika atakapo patikana
"Sisi kazi yetu ni kusimamia usalama na tumekagua Bus hilo tumejiridhisha tumeona hawezi kuendelea na safari ,ndipo tulipochukua hatua kwa usalama wa raia,niwaondoe hofu abiria kwamba Bus hilo tutaendelea kulishikilia watapata stahiki zao za kurudishiwa nauli ,"amesema.
Sisiwayah amesema Bus hilo ni kati magari yaliyopewa vibali vya muda na mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini LATRA kutoa huduma katika kipindi hiki cha cha sikukuu ya mwisho wa mwaka kuja Kilimanjaro kutokana na wingi wa abiria.



0 Comments