TAJIRI ESTHER LUXURY COACH ASEMA :DKT.MWIGULU LAMECK NCHEMBA SI MMILIKI WA MABASI YETU

 

 

MKURUGENZI  wa Kampuni ya mabasi ya ESTHER LUXURY COACH,Joseph Didas Ngeleuya amsema si kweli kuwa waziri Mkuu wa Tanzania ,Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba ni mmiliki wa mabasi yao.

Amesema hivi karibuni Kampuni yake imehusishwa kimakosa na baadhi ya viongozi wakuu wa kisiasa hapa nchini ikiwamo madai kuwa inamilikiwa na mheshimiwa waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini moshi hivi karibuni,Ngeleuya amesema kutokana na tetesi hizo zisizo za kweli kampuni yake imepata madhara makubwa wakati wa machafuko yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu oktoba 29 na bada ya uchaguzi ambapo waandamanaji walivamia kampuni yake na kuchoma mabasi sita na kuharibu mali nyingine nyingi.

“Napenda kuwajulisha waandishi wa habari na watanzania wote kwamba Esther Luxury Coach ni mali yangu na familia yangu bila kuhusishwa na kiongozi yeyote wa kisiasa au mtu mwingine yeyote nje ya familia yangu”

“Kampuni yangu ilisajiliwa tarehe 12 septemba 2024 ikiwa na wanahisa wawili tu ambaye ni mimi Joseph Didas Ngeleuya,mwanahisa wa pili ni  mke wangu Neema Peter Thomas”

“Kuhusu jina “ESTHER”tuliamua kulitumia kwa heshima ya mtoto wetu wa kwanza Esther Joseph Ngeleuya aliyezaliwa tarehe 2 septemba 2003 katika Hospital ya Taifa  Muhimbili Dar es salaam”

“Wakati tunaanzisha shughuli za usafrishaji miaka 15 iliyopita tulipitia changamoto nyingi za kibiashara na kifamilia ndipo tulipoamua kuipa biashara yetu jina la Esther Trans ambalo baadaye liliendelezwa na kusajiliwa rasmi kama Esther Luxury Coach mwaka 2024,huu ndiyo uhalisia na historia ya kampuni yetu” 

“Kwa masikitiko makubwa tunawasihi watanzania waache kufanya maamuzi ya kuharibu mali za watu kwa misingi ya tetesi na majungu,hasara tuliyopata ni kubwa sana na haiwezi kuelezeka kwa urahisi” 

“Kama kugekuwepo mashaka yoyote kuhusu umiliki wa kampuni hii ingekuwa rahisi sana kuthibitisha uweli kupitia BRELA ambapo huhifadhi taarifa rasmi za kampuni zote zilizosajiliwa nchini.



Post a Comment

0 Comments