OFISI YA CHAMA CHA MSINGI CHA KIRIMA BORO AMCOS
TUME ya maendeleo ya Ushirika nchini kuptia ofisi
ya Mrajis wa vyama vya ushirika imeifutilia mbali Bodi ya uangalizi ya Chama cha ushirika cha Kirima Boro Amcos baada
ya kutuhumiwa kujihusisha ya uuzaji wa sehemu ya shamba la Sangiti ambalo ni
mali ya ushirika.
Uamuzi huo ambao ulikuwa
unasubiliwa kwa hamu na wanachama wa chama hicho umekuja siku chache baada ya
kuwepo na kelele nyingi kutoka kwa wananchama hao wakilalamikia kitendo hicho.
Baada ya kuifutulia mbali
Bodi hiyo,Mrajis ametangaza kalenda ya uchaguzi wa Bodi mpya unaotarajiwa
kufanyika mapema mwezi huu huku akizuia viongozi waliokuwa kwenye Bodi hiyo kuwa
sehemu ya watakaochukua fomu.
Uamuzi huo umefanywa hivi
karibuni katika mkutano mkuu maalumu ulioitishwa na Mrajis mwenyewe na tayari
baadhi ya wanachama wameanza kuchukua fomu za kugombea nafasi za ujumbe wa Bodi
mpya.
Bodi huyo ilikuwa chini ya
mwenyekiti wake Hashim Michael Komu ambako wajumbe ni Alberith Joseph
Mushi,Abass Hatibu Kalanga,Aloyce August Kimaro na Mathew Ngowi.
Kabla ya uamuzi huo kufikiwa,mrajis alituma timu ya uchunguzi kuchunguza malalamiko ya wanachama hao ambao wanadai viongozi hao pia wameuza baadhi ya mali za ushirika ikiwamo trekta na jembe lake japo madai hayo yamekanushwa na viongozi hao
Kwa faida ya wasomaji wetu,tunakueletea taarifa yetu ya awali ambayo tuliichapisha hapa na namna shamba hilo lilivyopatikana kutoka kwa raia mmoja wa kigeni aliyekuwa akilitumia ambaye alishindwa kuliendeleza kutokana na kuzongwa na madeni yaliyotokana na mkopo wa Benki
NANI ANAUZA MASHAMBA YA CHAMA CHA USHIRIKA CHA KIRIMA BORO AMCOS KAMA
VIHAMBA ?
WANACHAMA wa
Chama cha msingi cha ushirika wa mazao cha Kirima Boro Amcos kilichopo wilaya
ya moshi Vijijini,wamepaza sauti kwa mamlaka za uchunguzi kupiga kambi kwenye
ofisi za chama hicho na kufanya uchuguzi juu ya madai ya viongozi wa muda wa
chama hicho kudaiwa kuuza mashamba ya chama hicho kama ardhi ya ukoo maarufu
kama vihamba kwa lugha ya kabila la Kichagga.
Wanadai kuwa viongozi hao
wamewauzia ardhi ya chama hicho watu mbalimbali wakiwamo
wanasiasa,wafanyabiashara wakubwa na watumishi wa umma jambo ambalo wanadai
haliendani na sera ya serikali katika mkakati wa kuendeleza ushirika nchini.
Timu yetu ya uchunguzi
iliyopiga kambi kwenye ushirika huo imeibua mengi ambayo bado tunayafanyia
uchunguzi ikiwamo majina ya waliouziwa ardhi hiyo Pamoja na kuwatafuta mmoja
baada ya mwingine ili kupata kauli zao juu ya kuuziwa ardhi ya wanaushrika.
Kwa faida ya wasomaji wetu,machi
21 mwaka 1967 vyama viwili vya msingi vya ushirika vya Kimasio na Kirima Boro
viliandika barua ya kuomba kununua shamba lililokuwa likimiliwa na raia mmoja
wa kigeni Tsoucas baada ya kubaini kuwa shamba hilo haliendelezwi .
“Vyama viwili vilivyotajwa
hapo juu vinayo heshima kubwa kununua shamba hilo kwa manufaa ya watu
wote,baada ya uchunguzi mwingi kwa wahusikao na shamba hilo ilionekana kuwa
liko chini ya ulinzi wa manager wa Standard Bank”,inasema barua hiyo na
kuongeza.
“Baada ya kumwona manager wa Bank alitoa dokezo kuwa shamba hilo ni ekari 450 na ni jumla ya sh,600,000,kwa kifupi,shamba hilo halina mastawisho yeyote bali kuna vyumba viwili tu(2),zaidi ya hapo tulikwisha julishwa kuwa alikuwa na deni la Bank jumla ya sh,15,000”.
Kuambatana na kima hicho
cha sh,600,000,tunakuomba shamba hilo lichukuliwe kama bei hiyo ni ya
halali,tunatumai kuwa ombi letu hili litafikiriwa kwa makini”,imehitimisha
barua hiyo ambayo nakala yake timu yetu ya uchunguzi inayo .
Kulingana na uchunguzi
wetu,Desemba 14 mwaka 2023 mwenyekiti wa Kijiji cha Boro,Laurent Mushi kwa
niaba ya wananchi wa kijiji hicho alimwandikia barua mkuu wa wilaya ya Moshi
akilalamikia mwenendo wa uongozi huo kuuza ardhi ya shamba la ushirika kama vihamba
akimuomba kuingilia kati lalamiko hilo na kumuomba azuie mpango wa
kugawa ardhi ya ushirika.
“Mh.Mkuu wa wilaya baadhi
ya wanakijiji wenye nia njema ya kudumisha amani wanakuomba uingilie kati
lalamiko hili na kuzuia mpango wa kugawa ardhi ya Ushirika inayosimamiwa na
Chama cha ushirika cha msingi cha Kirima Boro”.
Uratibu wa kumilikisha
vipande vidogo vidogo vya ardhi usimame na badala yake eneo libaki kwa ajili ya
Taasisi muhimu kwa umma mfano;Kituo cha Afya,Kituo cha Polsi Chuo cha ufundi
n.k”.
“Wanakijiji wamenieleza kuwa hofu yao ni kwamba mpango huu ukifanyika bila kuweka utaratibu wa kisheria wa kumilikisha ardhi ambayo ni mali ya Ushirika,viashiria vya ugomvi vinaweza kutokea katika shamba na kusababisha uvunjifu wa amani siyo tu kwa wanachama wa chama cha Ushirika cha msingi bali pia kwa wakulima ambao baba zao au mama zao ndio waliochangia fedha za kununua ardhi hiyo mwaka 1967 kutoka kwa wamiliki wa kigeni na wamekuwa wakijiuliza maswali yafuatayo…….”


.jpg)
.jpg)
0 Comments