MSOHI- KILIMANJARO
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Zuberi Abdallah Kidumo(wa tatu kutoka kushoto )akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwamo wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya muda mfupi baada ya kulakiapo kuashiria kuanza rasmi majukumu yake ya umeya.
NAAM,hivi
ndivyo unavyoweza kuanza kusema kwamba kurejea kwa kishindo kwenye nafasi yake
ya Umeya wa Manispaa ya Moshi kwa Mhandisi Zuberi Abdallah Kidumo ni ishara tosha ya kuwaziba
midomo wale waliokuwa katika harakati za kumchafua kwa namna mbali mbali na wengi
wakitumia mitandao ya kijamii kutekeleza nia yao ovu.
Zuberi Abdallah
Kidumo ni moja ya madiwani ndani ya Baraza la madiwani la manispaa ya moshi anayetajwa
kuwa na nidhamu ya hali ya juu ndani ya Baraza,kwa watumishi wa Halmashauri na ndani ya Chama chake cha Mapinduzi(CCM)nidhamu
inayotajwa kuwa imechangia kumbeba na kumbakisha kwenye nafasi yake.
Kwenye ukumbi mpya wa Mikutano wa Manispaa ya Moshi Alhamis ya Desemba 4 nderemo na vifijo vilisikika baada ya matokeo kutangazwa kuwa amepishwa kwa kura 28 za ndiyo na kuufanya ukumbi huo ambao ulijaa kupita kiasi kutawaliwa na kelele za pongezi.
Akizunguza
ara baada ya kulakiapo ,Kidumo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza madiwani
wenzake kwa kumpitisha kwa kura nyingi na kuahidi kushirikiana nao bega kwa
beka katika kuedneleza gurudumu la maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa
manispaa ya moshi.
“Kwa dhaani
hii mliyonipa nitashirikiana nanyi bega ka bega na nitashirikiana na serikli na
uogozi huu(wa manispaa ya Moshi)uliopo mbele yenu kuhakikisha tunakwenda
kuifanyiakazi ilani yetu ya uchaguzi ya chama cha mapinduziCCM)kama
tulivyowaahiidi wananchi “,alisema na kuongeza.
“Ni imani yangu kwamba kwa kura nyingi za ndiyo zilizopigwa hapa ndani ya ukumbi huu inatosha kabisa kuonesha Imani yenu kubwa mliyonayo kwangu na mimi nawahidi sitawangusha”,alisema.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Zuberi Abdallah Kidumo akizungumza muda mfupi baada ya kulakiapo kuashiria kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu yake kama meya .
Awali Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa(CCM) ilirejesha majina ya
madiwani watatu kwa ajili ya kupigiwa kura na madiwani kupata meya ambako yalikuwa
ni Benedict Mwashamba(Longuo B),Deo Mallya(Karanga) na Zuberi Abdallah Kidumo
ambaye ni dwani wa kata ya Njoro.
Katika
upigaji kura wa awali Zuberi Kidumo alipata kura 20 dhidi ya kura 10 alizopata mpinzani
wake Mwashamba huku Deo Mallya akijiengua dakika za mwisho baada ya kuwepo na tarifa
ya kufiwa na kaka yake.
Kidumo alichukua nafasi ya umeya katika serikali ya awamu ya tano baada ya aliyekuwa meya wa manispaa hiyo Juma Raibu Juma kuondolewa kwneey nafasi hiyo baada ya kuhusishwa na kashifa ya kuhudhulia sherehe ya kijana anayehusishwa kufungamana na ushoga.
KAZI IMEISHAAAA,NAAM,MSTAHIKI MEYA ZUBERI ABDALLAH KIDUMO(KULIA)AKIFURAHIA JAMBO NA ALIYEWAHI KUWA MEYA WA MANISPAA HIYO,JUMA RAIBU JUMA MUDA MFUPI BAADA YA WAWILI HAO KULA KIAPO NDANI YA UKUMBI WA MANISPAA YA MOSHI ALHAMISI DESEMBA 4,2025.
.jpg)







0 Comments