DIWANI ISSA WA KORONGONI AMWAGA VITENDEA KAZI KWA MAFUNDI GEREJI ,TAZAMA PICHA MBALI MBALI ZA DIWANI ISSA

 ZIARA YA DIWANI ISSA WA KATA YA KORONGONI KWA MAFUNDI GEREJI  KATIKA PICHA 


Diwani wa kata ya Korongoni Manispaa ya Moshi ,Issa Juma Bulilo ametoa msaada wa vitendeakazi kwa mafundi wa magari katika maeneo mbali mbali ndani ya kata yake ikiwa ni mkakati wa kuwawezesha kufanya kazi katika mazingira rafiki.
 

Diwani Bulilo alitembelea mafundi wa kuchomelea  waliopo eneo la Sido,mafundi Gereji kwa Mgosi mtaa wa Viwanda pamoja na mafundi gereji eneo la Banana mtaa wa vijana 

Akizungumza kwa nyakati tofauti na mafundi hao,diwani Issa pamoja na kuwashukuru kwa kushiriki vyema uchaguzi mkuu uliofanyika October 29 mwaka jana,aliahidi kuendelea kutatua changamoto wanazokabiliana nazo iikiwamo kuwa na maeneo rasmi ya kufanyia kazi zao.   

Diwani Issa aliwataka mafundi hao kumpa  ushirikiano akiamini kuwa msingi  wa maendeleo utatokana na wao kushirikiana .




MAFUNDI GEREJI BANANA KAZINI




Post a Comment

0 Comments