KATIKA Makala iliyopita tuliangazia changamoto wanazokabaliana nazo vijana wanaofanyakazi ya kubeba mizigo ya watalii ndani a Hifahdi ya Taifa ya Kilimanjaro(KINAPA)wanaojulikana kwa jina la wapagazi maarufu kama ‘wagumu’ ikiwamo maslahi duni licha ya kazi ngumu wanazozifanya.
Pamoja na Bunge kuidhinisha malipo mapya kwa wangozaji wageni,wapishi na wagumu kupitia tangazo la serikali (GN)namba 228 la mwaka 2008,bado makampuni mengi ya wakala wa utalii yamekuwa hayazingatiii viwango hivyo na kulipa kadri yanavyotaka.
Kwa mujibu wa Tangazo hilo,serikali iliweka kiwango cha dola 20 kwa siku kwa waongoza wageni(Guide)dola 15 kwa siku kwa wapishic na dola 10 ka siku kwa wagumu lakini mapaka leo malalamiko ni mengi juu ya viwango hivyo kutozingatiwa.
Vyama vya wapagazi ikiwamo Kilimanjaro Porters Association (KPA)Tanzania Porters Organazition(TPO) na Kilimanjaro Guide and Porters vinao mchango mkubwa sana wa kupigania maslahi ya vijana hawa.
Vyama hivi vya wapagazi vinaweza kushirikiana na serikali kuweka na kusimamia viwango vya malipo ya ujira kwa wapagazi, wapishi na waongoza watalii.
Vyama hivi pia vinaweza kushirikiana na serikali kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa makampuni ya wakala wa utalii yanawalipa wapagazi stahiki zao kama Tangazo la serikali linavyosema na kuchukua hatua kwa makampuni yanayowanyonya wapagazi,wapishi na waongoza wageni.
![]() |
| HAWA NDIYO WANAITWA WAGUMU |
Kutokana na changamoto hizo za maslahi kwa makundi hayo matatu,vyama vya wapagazi vinawajibika kutoa elimu kwa wapagazi kuhusu haki zao na jinsi ya kudai stahiki zao Pamoja na kutoa msaada wa kisheria katika kudai hali zao.
Kwa upande wa serikali inaweza kuweka sheria kali zaidi zinazolinda haki za wapagazi na kuhakikisha kuwa makampuni ya utalii yanawalipa stahiki zao kwa mujibu wa GN na kuchukua hatua pale yanapokiuka viwango hivyo vya mishahara.
JE
VYAMA HIVI VYA WAPAGAZI VINAWASAIDIA KWELI KUPAZA SAUTI?
Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wapagazi kwamba pamoja na uwepo wa vyama hivyo bado kilio cha mapujo ya mishahara hakijapatiwa ufumbuzi.
Mbali na hilo vijana hawa wanadai kuwa hata wanapopata changamoto za kiafya wakiwa kazini bado vyama hivyo vimekuwa na kigugumizi kuhakikisha makampuni wanayoyafanyia kazi yanawahudumia na kurejea katika hali zao za kawaida.
“Hebu waulize kila mwaka tunalipia vitambulisho vyetu vya mlimani hizo pesa zinafanya nini kama mtu unapata shinda mlimani na hakuna msaada wowote”,anasema kijana mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Kadama24blog imefanya uchunguzi na kubaii aslimia kubwa ya vijana hawa hawana bima ya afya ambayo inaweza kuwasaidia pale wanapopata changamoto za kiafya wakiwa kazini ikiwamo kuumia.
watalii wakipanda mlima kilimanjaro kuelekea kilele cha uhuru
USIKOSE MAKALA YETU IJAYO AMBAYO ITAELEZEA NAMNA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAPAGAZI WANAVYOSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZAO
Kadama24blog inaedelea na juhdi za kuwasiliana na viongozi wa vyama vya wapagazi kupata ufafanuzi kutoka kwao na namna wanavyoshughulikia changamoto za wagumu hao
Hii ni kutokana na juhudi zetu za muda mrefu kuomba kupata ufafanuzi kutoka kwao kushindikana




0 Comments