THERESIA KOMBA AONGOZA KINA MAMA WA UWT MANISPAA YA MOSHI KUTEMBELEA KINA MAMA WAJAWAZITO JENGO LA HUDUMA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO MAWENZI HOSPITAL,NI KATIKA KUMBUKIZI YA SIKU YA KUZALIWA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN

 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya wanawake (UWT)ya chama cha mapinduzi CCM Moshi Mjini,Theresia Komba amewaongoza viongozi wa ngazi mbali mbali wa jumuiya hiyo kutembelea kina mama wajawazito katika jengo la huduma ya afya ya mama na mtoto katika Hospital ya Rufaa ya mkoa ya mawenzi  na kuwapatia mahitaji mbali mbali ya kijamii pamoja na kuwapongeza kwa kujifungua salama.

Tukio hilo limeenda sanjari na kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan ambako matukio mawili makubwa yalifanyika ikiwamo kupanda miti eneo la jengo hilo pamoja na kukata keki.

Akizungumza mara baada ya kuwatembelea kina mama hao,mwenyekiti huyo wa Jumuiya hiyo ya wanawake ya chama cha mapinduzi moshi mjini,aliipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha huduma za afya nchini .


Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake (UWT)ya chama cha mapinduzi CCM Manispaa ya moshi,Theresia Komba(pichani) akipanda mti nje ya jengo la huduma ya afya ya mama na mtoto katika Hospital ya rufaa ya mkoa ya mawenzi ikiwa ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dtk.Samia Suluhu Hassan leo januari 27,2026.


Alisema hatua hiyo ya uwekezaji mkubwa kwenye kesta ya afya hasa huduma ya afya ya mama na mtoto imeweza kupungua kwa kiwango kikubwa vifo vya mama na mtoto.

Alitumia nafasi hiyo kupongeza huduma nzuri zinazotolewa na watumishi wa afya katika Hopsital hiyo ya rufaa ya mkoa ya mawenzi na kuwataka waendelee na moyo huo .

Mwenyekiti huyo alimtakia afya njema Mheshimiwa rais ili aweze kutimiza ndoto zake katika kuwahudumia watanzania.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani na mganga mfawidhi Hospital ya rufaa ya mkoa wa mawenzi ,Abilahi Issa alisema serikali imewekeza Zaidi y ash,Bilioni 1.9 kwa ajili ya mtambo wa kuzalisha hewa ya Oksijeni na kumaliza tatizo la kwend kununua maeneo mengine kwa gharama kubwa .

 Pia alisema kwa sasa Hospital ya mawenzi imemaliza tatizo la wagonjwa kwenda mbali na kutumia gharama kubwa kutafuta matibabu ya figo kwani huduma hiyo kwa sasa inapatikana kwenye Hospital hiyo.

Alisema uwekezaji uliofanywa na serikali ikiwamo kukamilika kwa jengo la huduma ya afya ya mama na mtoto ni kilelezo tosha kwa serikali katika kuboresha huduma za afya.

Kuhusu mpango wa Bima ya Afya kwa wote,Dkt.iss amesema Hospital hiyo imejipanga kuyapokea makundi maalum wakiwamo wenye ulemavu na wajawazito pamoja na wenye kipato cha chini.








 


Post a Comment

0 Comments